MBUNGE WA JIMBO AENDELEA KUKAGUA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SEKONDARI ZA KATA

Ukaguzi wa MIUNDOMBINU YA ELIMU ulioufanywa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwenye Sekondari ya Kata ya Kiriba, KIRIBA SECONDARY SCHOOL.

KIRIBA SEKONDARI ilianza kutoa ELIMU YA SEKONDARI Mwaka 2006. Kwa sasa ina Wanafunzi 672 na Walimu 21. Kuna UPUNGUFU wa Vyumba 2 vya Madarasa.
MATOKEO YA FORM IV YA MASOMO YA SAYANSI (2019)
Mwalimu Mkuu, Mwl Robertious Wanjara Bwire amesema kwamba MATOKEO YA MITIHANI YA MASOMO YA SAYANSI ya Mwaka jana (2019) ni MABAYA SANA. Fizikia (Physics) ilikuwa na Watahiniwa 4, mmoja (1) pekee alipata D. Kemia (Chemistry) ilikuwa na Watahiniwa 12, watatu (3) pekee walipata C. Biolojia (Biology) watahiniwa 99, waliopata B ni watatu (3) tu. Baadhi ya SABABU za msingi za MATOKEO MABAYA HAYO ni: (i) KUTOKUWEPO MAABARA yenye Miundombinu ya kujifunzia sayansi kwa vitendo (PRACTICALS)  na (ii) MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani.
WANANCHI NA SERIKALI WASHIRIKIANA KUTATUA MATATIZO HAYO
*MIRUNDIKANO Madarasani
Wananchi kutoka Vijiji 3 (Bwai Kwitururu, Bwai Kumusoma na Kiriba) vya Kata ya Kiriba WAMEKUBALIANA kuchangia NGUVUKAZI na FEDHA kujenga Vyumba 3 Vipya vya Madarasa. Kila Kijiji kinajenga jengo lake na kabla ya tarehe 30 March 2020, ujenzi huo uwe umekamilika na kutatua tatizo la MIRUNDIKANO madarasani.
SERIKALI Ilishachangia Tsh 37.5 Milioni kwa ajili ya ujenzi  na uboreshaji wa awali wa Vyumba vya Madarasa na ununuzi wa madawati na viti.
Jana, Jumatano, tarehe 4.3.2020, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo alikagua ujenzi mpya huo wa Vyumba 3 vipya na KUCHANGIA Jumla ya SARUJI MIFUKO 150 (kila Kijiji kimechangiwa Mifuko 50).
*MAABARA BORA YA KI-SAYANSI
Kiriba Sekondari inavyo Vyumba 3 vya MAABARA ya Fizikia, Kemia na Biolojia LAKINI MIUNDOMBINU ya NDANI ni hafifu sana au haipo. Kwa hiyo, Mbunge wa Jimbo AMEWASHAWISHI Wananchi wa Kata ya Kiriba KUANZA ujenzi wa KUBORESHA MAABARA 3 hizo.
SARUJI MIFUKO 60 inahitajika kujenga MEZA za TOFALI/BLOCK ndani ya Maabara hizi tatu (3). Mdau wa Maendeleo ya Kiriba amechangia SARUJI MIFUKO 35 na Mbunge wa Jimbo amechangia SARUJI MIFUKO 25. Uboreshaji wa Miundombinu ya ndani ya Maabara tatu (3) za Sekondari hii umepangwa UKAMILIKE kabla ya tarehe 30 April 2020.
WAZALIWA wa Kata ya KIRIBA na WALIOSOMA Kiriba Sekondari wanaombwa WAJITOKEZE KUCHANGIA UBORESHAJI wa miundombinu ya ndani ya MAABARA hizi tatu
Mawasiliano ya MICHANGO
Headmaster:
0787 015 489
Mtendaji Kata (WEO):
0758 023 124
0629 537 798
SAYANSI NI CHIMBUKO LA UCHUMI WA KISASA NA USTAWI WA JAMII ZOTE DUNIANI KOTE