ZAHANATI YA KIJIJI CHA MASINONO KUPANULIWA NA KUWA KITUO CHA AFYA CHA KATA YA BUGWEMA

MKUTANO wa WANANCHI wa Kata ya Bugwema na MBUNGE wao, Prof Sospeter Muhongo kwenye eneo la (ujenzi) Zahanati ya Masinono, Kata ya Bugwema.

SERIKALI imetoa Tsh Milioni 400 kupanua ZAHANATI ya Kijiji cha Masinono na kuwa KITUO CHA AFYA cha Kata ya Bugwema.
WANANCHI na VONGOZI wa Kata ya Bugwena na Halmashauri yao WANAISHUKURU sana SERIKALI yao na WAMEHAIDI kushirikiana nayo kukamilisha MRADI huu.
Jana, Jumatatu, tarehe 2.3.2020, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ALITEMBELEA Zahanati ya Masinono na KUONGEA na WANANCHI kuhusu UPANUAJI wa Zahanati hiyo.
Diwani wa Kata ya Bugwema, Mhe Ernest Maghembe amesema, MAJENGO MAPYA yatakayojengwa ni: (i) Wadi la Mama & Mtoto, (ii) Jengo la Upasuaji (theatre) (iii) Maabara, (iv) Jengo la kufulia nguo, (v) Kichomea taka na (vi) Nyumba ya kutunza maiti (mortuary). Mindombinu mizuri ya Maji Safi na Taka itawekwa.
MICHANGO YA WANANCHI
Kata ya Bugwema inaundwa na VIJIJI 4 vya Bugwema, Kinyang’erere,  Masinono na Muhoji.
* NGUVUKAZI – kila Kijiji kimepangiwa siku za kusomba mawe, mchanga, maji, n.k.
* Kila Kijiji kitachangia Tsh 33, 437, 500 ili kupata Jumla ya Tsh 133,750,000 kwa ajili ya ujenzi huu.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
* Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Jimbo ametoa AHADI ya KUCHANGIA UJENZI huo Mwezi ujao (April, 2020) atakaporudi hapo KUKAGUA ujenzi wa KITUO hicho cha AFYA.
Mbunge huyo amewaeleza Wananchi wa Kata ya Bugwema kwamba alichangia SARUJI MIFUKO 400 wakati wa UBORESHAJI wa Miundombinu ya  KITUO cha AFYA MURANGI na kukipatia Gari la Wagonjwa  (Ambulance) la kisasa sana. Vilevile, alichangia SARUJI MIFUKO 400 wakati wa upanuaji wa Zahanati ya Mugango kuwa KITUO cha AFYA MUGANGO. Na hapa napo, Mbunge huyo alitoa Gari la Wagonjwa (Ambulance).
ZAHANATI ya Masinono inayopanuliwa kuwa Kituo cha Afya tayari Mbunge wa Jimbo aliishaipatia Gari la Wagonjwa (Ambulance).
MIUNDOMBINU YA HUDUMA ZA AFYA NA MAGARI YA WAGONJWA JIMBONI MWETU.
* HOSPITAL ya Wilaya: inajengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti.
* VITUO VYA AFYA vinavyotoa huduma ni viwili (2): Kata za Murangi na Mugango
* VITUO VYA AFYA vinavyojengwa ni viwili (2). Kata za Bugwema na Nyambono
* ZAHANATI zinazotoa huduma: 24 za Serikali na 4 za Binafsi
* ZAHANATI MPYA zinazojengwa ni kumi na tatu (13).
* MAGARI YA WAGONJWA (Ambulances) ni matano (5). Yote yalitolewa na Mbunge wa Jimbo.