SHEREHE ZA UZINDUZI WA BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL ZAFANA SANA

Wananchi na Mbunge wa Jimbo katika Sherehe za Uzinduzi wa Busambara Secondary School

Jumamosi, 29.2.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
HATIMAE Kata ya Busambara iliyokuwa haina Sekondari yake IMEFANIKIWA KUJENGA na tayari Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza wameanza MASOMO yao Shuleni hapo.
KATA MOJA tu kati ya Kata 21 za Jimbo la Musoma Vijijini ndiyo haina Sekondari yake. Hata hivyo, Kata hiyo (IFULIFU) inajenga Sekondari mbili (Nyasaungu & Ifulifu Secondary Schools) kwa wakati mmoja na zitakuwa tayari kuchukua Wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ifikapo Juni 2020.
Kwa sasa, Jimbo lina Sekondari 20 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi. Sekondari Mpya zinazojengwa ni 5: (i) Kigera (Kata ya Nyakatende), (ii) Nyasaungu (Kata ya Ifulifu), (iii) Ifulifu (Kata ya Ifulifu inajengwa Kijijini Kabegi), (iv) Bukwaya (Kata ya Nyegina) na (v) Seka (Kata ya Nyamrandirira). Kata (3) nyingine nazo zimepanga kutatua matatizo ya umbali mrefu na mirundikano madarasani kwa kujenga Sekondari mpya ndani ya Kata zao.
Leo, Jumamosi, tarehe 29.2.2020 JIWE LA MSINGI na UZINDUZI wa Busambara Secondary School umefanyika Kijijini Kwikuba na MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo. Hii SEKONDARI MPYA ni ya Vijiji 3 (Kwikuba, Maneke na Mwiringo).
MAOTEO ni kwamba mwakani (2021) takribani WANAFUNZI 270 wanategemewa kuanza Kidato cha Kwanza Shuleni hapo. Kwa hiyo ujenzi kwa kasi kubwa ni muhimu.
Wananchi na Mbunge wa Jimbo watafanya KIKAO cha MUENDELEZO WA UJENZI wa Miundombinu ya Sekondari hii tarehe 6 Machi 2020, Saa 10 Alasiri, Shuleni hapo.