KIRIBA SEKONDARI – UPUNGUFU WA VYUMBA VYA MADARASA KUTATULIWA KWA USHIRIKIANO WA  WANANCHI NA SERIKALI

Ujenzi wa Vyumba VIPYA 3 vya KIRIBA SECONDARY SCHOOL ya Kata ya Kiriba

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Mkuu wa Kiriba Sekondari, Mwalimu Robertious Wanjara Bwire amesema kwamba Sekondari hiyo ilianzishwa Mwaka 2006 na ina jumla ya WANAFUNZI 672 na WALIMU 21. Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 18, vilivyopo ni 16 kwa hiyo UPUNGUFU ni VYUMBA 2.
WANANCHI wa Kata ya Kiriba inayoundwa na Vijiji vitatatu (3) vya Bwai Kumusoma, Bwai Kwitururu na Kiriba wameanza ujenzi wa Vyumba VIPYA vitatu (3) vya Madarasa ili KUTOKOMEZA KABISA tatizo la MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani.
Akizungumza na Msaidizi wa Mbunge katika eneo la ujezi shuleni hapo, Mtendaji Kata (WEO) ya Kiriba, Ndugu Pendo Isack amesema ujenzi wa VYUMBA VIPYA hivyo unaendeshwa na Vijiji vyote vitatu ambapo kila Kijiji kinajenga Chumba kimoja (1) cha Darasa.
Mtendaji Kata huyo ameongezea kuwa, ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi ujao (30 March 2020) ili kuharakisha matumizi yake na KUONDOA MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani
Aidha Mkuu wa Sekondari hiyo AMEISHUKURU sana SERIKALI iliyochangia Tsh 37.5 Milioni kwa ujenzi huo (na ununuzi wa madawati na viti). Vilevile, anawashukuru sana Wanavijiji wa Kata ya Kiriba, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Mbunge wa Jimbo kwa USHIRIKIANO wao na MICHANGO yao inayokusudia kuondoa kabisa kero ya MISONGAMANO ya Wanafunzi madarasani.
Kwenye ujenzi huu wa Vyumba Vipya 3 vya Madarasa, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo atachangia Jumla ya SARUJI MIFUKO 150, yaani kila Kijiji kitakabidhiwa Saruji Mifuko 50. Makabidhiano hayo yatafanyika tarehe 4.3.2020, siku ambayo Mbunge huyo atakagua ujenzi wa Maabara na Vyumba VIPYA vya Madarasa Shuleni hapo.
MICHANGO YA AWALI YA MBUNGE WA JIMBO ni:
(i) Vitabu vingi vya Maktaba
(ii) Saruji Mifuko 100
(iii) Mabati 54
(iv) Rangi Ndoo 20
WAZALIWA WA KATA YA KIRIBA wanaombwa waendelee KUCHANGIA UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA KIRIBA SECONDARY SCHOOL