VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VINAVYOJENGWA VITAWATOA WANAFUNZI CHINI YA MITI

ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa ya S/M Wanyere B, Kijijini Wanyere, Kata ya Suguti

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijiji lenye Vitongoji 374, Vijiji 68 na Kata 21 lina jumla ya SHULE za MSINGI 111 za Serikali na 3 za Binafsi. Kuna UPUNGUFU mkubwa wa Vyumba vya Madarasa kwa baadhi ya Shule hizi za Msingi.
Kutokana na umbali mrefu wa kutembea na mirundikano madarasani, WANAVIJIJI kwa kushirikiana na SERIKALI, MADIWANI, MBUNGE wa Jimbo na WADAU wengine wa Maendeleo WAMEAMUA kujenga SHULE SHIKIZI MPYA 11 ambazo hapo baadae zitapanuliwa na kuwa SHULE za MSINGI kamili na zinazojitegemea.
KIJIJI CHA WANYERE CHAFUFUA MIRADI YA UJENZI WA VYUMBA VYA MADARASA
Kijiji cha Wanyere, Kata ya Suguti KIMEAMUA kuendeleza MIRADI ya ujenzi wa MIUNDOMBINU ya SHULE zake za MSINGI baada ya kusuasua kwa zaidi ya miaka miwili – UONGOZI MPYA wa Serikali ya Kijiji ndio unafufua miradi hii.
Kijiji cha Wanyere kina VITONGOJI 6, ambavyo ni:
Mwikoro, Komesi, Mururangu, Miulu, Murugee na Ambagai. Kijiji hiki kina jumla ya Shule za Msingi 3 ambazo ni: S/M Wanyere, S/M Wanyere B, na S/M Murugee.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Wanyere, Ndugu Thomas Musiba amesema ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa umeanza kwa MPANGILIO ufuatao:
 S/M WANYERE B
(i) Vitongoji vya Mwikoro na Komesi  wanaezeka Boma la Vyumba Vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu.
(ii) Vitongoji vya Mururangu na Miulu  wanajenga Boma la Vyumba Vipya  2 vya Madarasa na tayari limefika kwenye renta.
UJENZI WA NYUMBA ZA WALIMU
S/M MURUGEE
Vitongoji vya Murugee na Ambagai vinajenga NYUMBA MPYA 2 za WALIMU.
Mwenyekiti huyo wa Kijiji cha Wanyere amesema kuwa ujenzi wote huo utakamilika ifikapo tarehe 1 Machi 2020.
Diwani wa Kata hiyo ya Suguti, Mhe Denis Ekwabi amemshukuru sana Mbunge wa Jimbo lao kwa jitihada kubwa anazozifanya Jimboni katika kutekeleza ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020). Diwani huyo ameomba WADAU wa Maendeleo wakiwemo WAZALIWA wa Kata ya Suguti kujitokeza kuchangia ujenzi huo.
MICHANGO ALIYOKWISHATOA MBUNGE WA JIMBO
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ametoa MICHANGO ifuatayo kwa Shule zote (3) za Msingi za Kijiji cha Wanyere:
(i) VITABU vingi vya MAKTABA kwa Shule zote 3.
S/M WANYERE
(ii) Madawati 71
(iii) Saruji Mifuko 25
S/M WANYERE B
(iv) Madawati 100
(v) Saruji Mifuko 85
(vi) Mabati 108 (Mfuko wa Jimbo)
S/M MURUGEE
(vii) Madawati 122
(viii) Saruji Mifuko 50  (Mfuko wa Jimbo)
WANYERE WAMEAMUA KUTATUA TATIZO LA MIUNDOMBINU YA ELIMU KWENYE SHULE ZAO – KARIBU USHIRIKIANE NAO.