SHULE YA MSINGI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 1942 YAOMBA MICHANGO ZAIDI KUTOKA KWA MBUNGE WA JIMBO

ufyatuaji wa matofali ya Shule ya Msingi BUTATA iliyoanza KUTATUA TATIZO la UKOSEFU wa Vyumba vya Madarasa na Ofisi za Walimu Shuleni hapo.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
SHULE YA MSINGI BUTATA ya Kijiji cha Butata, Kata ya Bukima iliyofunguliwa Mwaka 1942 kwa sasa ina WANAFUNZI 551, ambapo Wanafunzi wa Darasa la Kwanza (2020) ni 62 na uandikishaji unaendelea.
S/M BUTATA (B) iliyofunguliwa Mwaka 2014 ina Jumla ya WANAFUNZI 620, ambapo Darasa la Kwanza (2020) ni 80 na uandikishaji unaendelea.
Mwalimu Mkuu wa S/M Butata, Mwl Nancy Lema amesema WANAFUNZI 210 wanasomea nje CHINI YA MITI kwa sababu ya UKOSEFU wa Vyumba 6 vya Madarasa. Mwl Zablon Sehaba, Mwalimu Mkuu S/M Butata B amesema WANAFUNZI ZAIDI ya 221 wanasomea nje CHINI YA MITI kwa sababu hiyo hiyo. MVUA zinaponyeesha MISONGAMANO MADARASANI inakuwa mikubwa mno hadi kufikia Wanafunzi zaidi ya 100 kwenye Chumba kimoja cha Darasa.
UAMUZI WA KUTATUA TATIZO LA UKOSEFU WA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE ZOTE MBILI ZA KIJIJI CHA BUTATA
S/M BUTATA
*Uongozi wa Shule UMEAMUA kuanza ujenzi wa Vyumba 2 VIPYA vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu kwa kutumia na kufuata TARATIBU zilizowekwa za RUZUKU (Elimu bila Malipo) wanayopewa na Serikali. Wanaomba WANANCHI na  Mbunge wao Prof Sospeter Muhongo WAUNGANE nao kwenye ujenzi huu. Mbunge huyo AMEKUBALI kuungana nao na ataanza kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 50.
S/M BUTATA B
* Shule inasubiri Serikali ya Kijiji iwapatie ENEO LA UJENZI na wao waanze. Vilevile, Wananchi na Mbunge wao wanaombwa washirikiane nao muda ukiwadia.
MICHANGO iliyokwishatolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwa Shule zote mbili za Kijijini Butata ni kama ifuatavyo:
 S/M BUTATA:
*Madawati 21
*Vitabu vingi vya Maktaba
*Mfuko wa Jimbo – Mabati 54
S/M BUTATA B
*Madawati 65
*Vitabu vingi vya Maktaba
*Saruji Mifuko 60
*Mfuko wa Jimbo – Mabati 54
WADAU WA MAENDELEO WANAOMBWA KUCHAGIA UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA MADARASA
*WAZALIWA wa Kijiji cha Butata WANAOMBWA WACHANGIE ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa na Ofisi za Walimu za  Shule 2 hizo za Kijijini mwao.
*WADAU wengine wa Maendeleo nao wanaombwa wachangie ujenzi huo.