MRADI WA BMZ (UJERUMANI) WASAIDIA WATOTO WENYE ULEMAVU KWENYE KATA 10 ZA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

MRADI wa BMZ (Ujerumani) wa UGAWAJI wa Vifaa vya Shule na Chakula kwa Wanafunzi wenye ULEMAVU kutoka kwenye Kata 10 za Jimbo la Musoma Vijijini.

WATOTO WENYE ULEMAVU ndani ya Kata 10 za Jimbo la Musoma Vijijini  WAMEPEWA VIFAA VYA SHULE kutoka Mradi wa BMZ (Ujerumani) ulio na Ofisi zake kwenye Hospitali Teule ya SHIRATI, Wilaya ya Rorya.
BMZ (The Federal Ministry of Economic Cooperation and Development, formed in 1961) ya UJERUMANI ina MRADI wa KUHUDUMIA na KUTOA MATIBABU kwa Watu wenye ULEMAVU kwenye Wilaya 2 za Mkoa wa Mara.
MRADI huu ni wa USHIRIKIANO kati ya BMZ (Ujerumani) na Hospitali Teule ya Kanisa la Mennonite (KMT) la SHIRATI ambao unasaidia na kuwezesha WATU WENYE ULEMAVU kutoka KATA 10 za Wilaya ya Rorya na KATA 10 za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
MRADI HUU hutoa Vifaa vya Kimatibabu vinavyohitajika kwa Watu wenye ULAMAVU, MITAJI ya kuwawezesha kiuchumi na VIFAA vya SHULE kwa Wanafunzi wenye ULEMAVU. Hayo yameelezwa na Meneja wa Mradi wa BMZ, Ndugu Niwaely Sandy.
Hivi karibuni, kama ilivyo kawaida ya MRADI huu mara tu SHULE ZINAPOFUNGULIWA, Wanafunzi wenye ULEMAVU wamepewa:
*Vifaa vya Shule vikiwemo mabegi, madaftari na kalamu
* Vyakula – mchele, maharage na sukari
* Baadhi ya Wanafunzi hao watafanyiwa UPASUAJI wa MAREKEBISHO kwenye Hospitali Teule ya Shirati.
Wanafunzi wenye ULEMAVU waliopewa vifaa na chakula kutoka MRADI wa BMZ ni wa kutoka KATA za Bugwema, Bukima, Bukumi, Bwasi, Kiriba, Makojo, Murangi, Nyambono, Nyamrandirira na Suguti.
WANANCHI na VIONGOZI wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUSHUKURU SANA Mradi wa BMZ (Ujerumani)  kwa kutoa MISAADA ya Vifaa, Vyakula, Matibabu ya bure na MITAJI kwa Watu wenye ULEMAVU ndani ya Kata 10 zilizoko kwenye MRADI huu.