MAZAO YA VIKUNDI VYA KILIMO YAPATA KWA URAHISI MASOKO YA NDANI

Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wakiwa na mavuno yao ya MATIKITI. Mfanyabiashara, Ndugu Salha Mohamed ameenda Kijijini Bwasi kununua MATIKI ya Kikundi hicho.

Jumapili, 8.12.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
KIKUNDI cha NO SWEAT NO SWEET cha Kata ya Bwasi kinaendelea kunufaika na MRADI wa KILIMO baada ya kujifunza kulima mwaka mzima, yaani kwa vipindi vya kiangazi na masika.
Mwenyekiti wa KIKUNDI hiki, Ndugu Goodluck Wambwe ameeleza kuwa wako kwenye KILIMO cha BIASHARA cha Mazao ya MAHINDI, MATIKITI, VITUNGUU na NYANYA.
Kiongozi huyo ameongeza na kusema kwamba, WAMEFANIKIWA KUNUNUA MASHINE YA PILI ya Umwagiliaji.
Vilevile, KIKUNDI hiki KIMEFANIKIWA kufungua AKAUNTI BENKI, kununua SHAMBA jingine, kulipa ADA za masomo ya watoto wao na kuhudumia FAMILIA zao kwa ubora zaidi.
Ndugu Salha Mohamed (pichani), Mfanyabiashara kutoka Kijiji cha Bukima anashukuru sana kwa VIKUNDI vya KILIMO hasa vya UMWAGILIAJI kujitokeza kwa wingi JIMBONI humo na  kulima MAZAO ya BIASHARA.
“Kwa sasa tumepunguza sana gharama za kusafiri nje ya Jimbo letu kwenda kununua MAZAO ya BIASHARA. Bidhaa nyingi tunazipata ndani ya Jimbo letu”, alisema Mfanyabiashara huyo, Ndugu Salha Mohamed.
Ndugu Gustavu Tesha, Kaimu Afisa Kilimo wa Kata ya Bwasi amekuwa akitoa elimu juu ya KILIMO cha UMWAGILIAJI na kufanikiwa kuongeza idadi ya VIKUNDI vya KILIMO cha  UMWAGILIAJI ndani na nje ya Kata hiyo.
Wanachama na Viongozi wa Kikundi cha NO SWEAT NO SWEET wanamshukuru sana Mbunge wao  Profesa Sospeter Muhongo kwa kuwapatia MASHINE ya kwanza ya UMWAGILIAJI. Hiki Kikundi ni moja ya VIKUNDI 15 vilivyopewa MASHINE za UMWAGILIAJI na mbegu Mwaka 2016. Vifaa hivi vilinunuliwa kutoka kwenye Fedha za MFUKO wa JIMBO.
VIKUNDI VYA KILIMO CHA UMWAGILIAJI vinazidi kuongezeka ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
Tarehe 24.12.2019 (Christmas Eve) Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ATATOA ZAWADI YA KRISMASI ya PLAU (jembe la kukokotwa na ng’ombe) kwa VIKUNDI 14 kutoka VIJIJI 14 vya Jimbo la Musoma Vijijini.