BARAZA LA MADIWANI LAFANYA UAMUZI WA KUJENGA VETA KWENYE HALMASHAURI YAO

Wajumbe wa BARAZA la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma. Kikao kilifanyika tarehe (6.12.2019) kwenye Ukumbi wa Kanisa Katoliki Mugango.

BARAZA la MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma  LIMEFANYA UAMUZI MUHIMU kwa Maendeleo ya Wananchi wa Halmashauri hiyo yenye Jimbo la Musoma Vijijini.
JIMBO hilo lina Kata 21, Vijiji 68 na Vitongoji 374.
Shule za Msingi za Serikali ni 111, za Binafsi ni 3 na Shule Shikizi ni 10. Jimbo lina Sekondari za Serikali/Kata 18, za Binafsi 2 na Sekondari Mpya zinazojengwa ni 9. WINGI wa WAHITIMU wa Shule zote hizi WANAHITAJI FURSA ZAIDI za kujiendeleza kiuchumi.
WILAYA ya Musoma yenye Jimbo la Musoma Vijijini na Jimbo la Musoma Mjini inayo VETA MOJA iliyoko Musoma Mjini. Kwa hiyo UAMUZI wa leo (6.12.2019) wa BARAZA la MADIWANI wa Jimbo la Musoma Vijijini UNASTAHILI PONGEZI NYINGI sana – KUPANUA WIGO WA FURSA ZA  WAHITIMU kujiendeleza kiuchumi.
VETA itakayojengwa itazingatia hali halisi ya Sekta Kuu za Uchumi (k.m. Uvuvi, Kilimo na Ufugaji) wa Jimbo la Musoma Vijijini.