PROF MUHONGO AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI NA KUSISITIZA UKAMILISHWAJI WA MIRADI YA MAENDELEO

Jumapili, tarehe 17.11.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo AMEZINDUA Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwenye KATA ya KIRIBA yenye Vijiji 3.
Mbali ya kuelezea MAFANIKIO yaliyopatikana kwa UTEKELEZAJI MZURI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Muhongo AMEWASHAWISHI Wananchi wa Kata ya Kiriba KUONGEZA KASI ya kutekeleza Miradi yao ya Maendeleo kwa kushirikiana na SERIKALI yao na Wadau wengine wa Maendeleo.
WAGOMBEA wa CCM wa nafasi mbalimbali za uongozi wa Serikali za Mitaa WAMEAHIDI kushirikiana vizuri na WANANCHI, SERIKALI na WADAU wengine wa Maendeleo KUKAMILISHA Miradi iliyopo na KUANZA Miradi mipya.
VIONGOZI Wateule wa Kata ya Kiriba WAMEAHIDI kuongeza kasi ya Ukamilishwaji wa MAABARA 3 (Physics, Chemistry and Biology) za Kiriba Secondary School. Kila Kijiji kitakamilisha Maabara moja.
VIONGOZI Wateule wa Kata ya Kiriba WAMEAHIDI kuharakisha ujenzi wa Vyumba VIPYA vya Madarasa na kwamba HAKUNA WANAFUNZI KUSOMEA CHINI YA MITI ndani ya Kata hiyo.
Kijiji cha Chanyauru ndicho pekee hakina Zahanati ndani ya Kata ya Kiriba. VIONGOZI Wateule wa Kijiji hicho WAMEAHIDI kuongeza kasi ya ujenzi wa Zahanati yao.
UZINDUZI wa Kampeni wa Kata ya Kiriba UMEFANIKIWA SANA kwani VIONGOZI mbalimbali wa CCM na WAGOMBEA wateule wa CCM wamesisitiza umuhimu wa USHIRIKIANO MZURI kwenye UTEKELEZAJI wa Miradi yao ya Maendeleo.