WANANCHI WAAMUA KUUNGANA NA SERIKALI KWENYE UJENZI WA HOSPITAL YA  WILAYA

SARUJI (Mifuko 100) iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo kwaajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea KUTOA SHUKRANI  zao za DHATI kwa SERIKALI yao kwa kuwapatia Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kijijini Suguti kwenye Kitongoji cha Kwikonero.
WANANCHI wa Vijiji vyote 68 vya Jimbo la Musoma Vijijini WAMEKUBALI kuchangia Tsh Milioni 2 kila KIJIJI ili kuharakisha ukamilishwaji wa ujenzi wa HOSPITALI hiyo.
Hadi leo hii, 13.11.2019 MAJENGO yafutayo yako kwenye hatua ya ukamilishwaji:
(i) OPD, (ii) Pharmacy, (iii) X-Ray, (iv) Maabara, (v) Wadi la Mama&Mtoto, (vi) Utawala, (vii) Ufuaji (laundry)
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameungana na WANANCHI wenzake wa Jimboni mwao kuchangia ujenzi huu na leo amechangia SARUJI MIFUKO 100.
MAFANIKIO ya kazi nzuri za MRADI huu yanatokana na UONGOZI na USIMAMIZI mzuri na wenye ubunifu mkubwa wa Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Anney Naano, Mkurugenzi Mtendaji (DED), Ndugu John Lipesi Kayombo pamoja Wafanyakazi kwenye Ofisi zao.
HONGERENI SANA WANANCHI NA VIONGOZI WA MUSOMA DC.