SEKONDARI MPYA MBILI (2) NI LAZIMA ZIKAMILIKE LA SIVYO MSONGAMANO MADARASANI HAUTAEPUKIKA

DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL ya Kata ya BUGOJI (Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugoji) kazi ya ufyatuaji wa MATOFALI kwaajili ya ujenzi wa MATUNDU ya VYOO na VYUMBA vya MAABARA 3 inaendelea.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 na Vitongoji 374 lina SEKONDARI 18 za Kata /Serikali na SEKONDARI 2 za Binafsi (Madhahebu ya Katoliki & SDA).
WANAVIJIJI kwa kushirikiana na SERIKALI yao na WADAU wengine wa Maendeleo wanajenga SEKONDARI MPYA 9.
MATOKEO ya MITIHANI ya Darasa la VII ya Mwaka huu (2019) YANATULAZIMISHA KUONGEZA SEKONDARI MPYA 2-3 ili KUEPUKA MSONGAMANO wa Wanafunzi wa Kidato  cha Kwanza (Form I) kwenye SEKONDARI 18 zilizopo.
UFAULU WA KATA ZISIZOKUWA NA SEKONDARI ZAO
*Kata ya BUGOJI 141
*Kata ya NYAMBONO 149
(Nyambono Secondary School ni ya Kata 2: Nyambono & Bugoji)
*Kata ya BUSAMBARA 142
*Kata ya IFULIFU 130
(Kijiji cha Nyasaungu, Kata ya Ifulifu kinajenga Sekondari yake chenyewe, Wamefaulu 55)
WANAFUNZI wa Sekondari wa Kata ya BUGOJI (Vijiji 3) WANAENDA masomoni kwenye Sekondari ya Kata ya NYAMBONO (Vijiji 3). Kwa hiyo Mwakani (Januari 2020) JUMLA YA WANAFUNZI 290 wanapaswa kuanza Form I hapo Nyambono Secondary School! MSONGAMANO na MRUNDIKANO wa HALI JUU! TUSIKUBALI!
SULUHISHO: Dan Mapigano Memorial Secondary School IKAMILIKE HARAKA na Januari 2020 ichukue Wanafunzi wa Form I:
(i) Vyumba Vipya 5 vya Madarasa vimeishakamilika
(ii) Madawati  200 tayari yamewekwa Madarasani
(iii) Ofisi Mpya 2 za Walimu zimekamilika
(iv) Ujenzi wa Vyoo Matundu 10 ya Wanafunzi na 2 ya Walimu UTAKAMILIKA ndani ya WIKI MOJA ijayo.
(v) Ujenzi wa Maabara 3 (Physics, Chemistry na Biology) UNAENDA KWA KASI..msingi umejengwa na matofali yanafyatuliwa. Ujenzi utakamilika Disemba 2019.
(vi) Ujenzi wa Nyumba ya Walimu (two in one) umeanza, utakamilika Disemba 2019.
FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO (Saruji Mifuko 290 na Nondo 100) umeongeza kasi ya UKAMILISHAJI wa MAJENGO ya Dan Mapigano Memorial Secondary School.
MAKTABA ya KISASA itajengwa hapo Shuleni Mwakani (2020). Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEAHIDI kuendesha HARAMBEE ya ujenzi huo na AMEAHIDI kujaza VITABU kwenye MAKTABA hiyo ya MFANO.
WALIOTOA AHADI YA KUCHANGIA ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School WANAOMBWA WAKAMILISHE AHADI ZAO.
TAARIFA za ujenzi wa Sekondari Mpya za BUSAMBARA (inajengwa na Kata yenye Vijiji 3) na  NYASAUNGU (inajengwa na Kijiji kimoja cha Nyasaungu), nazo ZITATOLEWA.