SERIKALI YAENDELEA NA MATAYARISHO YA MRADI MKUBWA WA MAJI NDANI YA JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Wataalamu wakipima Eneo ambalo TANKI la usambazaji MAJI litajengwa.

MRADI WA MAJI WA MAZIWA MAKUU
Timu ya WATAALAMU wa MAJI kutoka Wizara ya Maji na Umwagiliaji na Ofisi ya Wilaya ya RUWASA (Wakala wa Maji Vijijini) WAMEANZA HATUA YA PILI ya Utekelezaji wa MRADI  huu, ambayo ni UPIMAJI wa Maeneo ambapo MIUNDOMBINU ya USAMBAZAJI MAJI itajengwa ndani ya VIJIJI 33 vya Jimbo la Musoma Vijijini.
VIJIJI hivyo 33  vilivyoko karibu na Ziwa Viktoria ndivyo vitakuwa vya kwanza
kusambaziwa MAJI ya MRADI huu.
WATAALAMU hao wameanza kazi zao kwenye Vijiji vya Kurukerege na Mkirira, Kata ya Nyegina. Diwani wa Kata hiyo, Mhe Rajabu Majira Mchele aliambatana na Wataalamu hao walipokuwa kazini kwenye Kata yake.
Kazi zinaendelea kwenye Vijiji 33 vya Jimbo la Musoma Vijijini vilivyoko kwenye MRADI wa MAJI wa MAZIWA MAKUU.
SERIKALI INATIMIZA AHADI YAKE YA KUSAMBAZA MAJI SAFI NA SALAMA VIJIJINI – Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kuiomba SERIKALI yao ikamilishe MRADI huo mapema iwezekanavyo.