KARIBU TUKAMILISHE MAJENGO YA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL

Moja ya majengo yanayokamilishwa sasa ni pamoja na Vyoo vya Wanafunzi na Waalimu

Wananchi wa Kata ya Bugoji WANASHIRIKIANA vizuri sana na SERIKALI yao, na WADAU wengine wa Maendeleo, akiwemo Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo,  KUHAKIKISHA kwamba Sekondari yao ya Kata inafunguliwa Januari 2020.
Vilevile, WAZALIWA wa Kata ya Bugoji yenye Vijiji 3 (Kaburabura, Kanderema na Bugoji) WANAENDELEA KUCHANGIA ujenzi wa Sekondari hiyo iliyoanza kujengwa Disemba 2018.
Kata hiyo HAINA SEKONDARI, kwa hiyo Watoto wao wanatembea umbali usiopungua kilomita 4 kwenda masomoni kwenye Sekondari ya Kata jirani (Nyambono). Hivyo, Nyambono Secondary School ina msongamano mkubwa madarasani kwa Wanafunzi kutoka Kata 2 hizo (Nyambono na Bugoji).
MAJENGO YALIYOKAMILISHWA
* Vyumba 5 vya Madarasa
* Ofisi 2: Mwalimu Mkuu (1) na Walimu (1)
MAJENGO YANAYOKAMILISHWA
* Vyoo vya Wanafunzi na Walimu (misingi tayari imejengwa)
* Maabara:  (misingi inachimbwa)
Diwani wa Kata Mhe Ibrahimund Malima, Mtendaji wa Kata, Ndugu Edina Kurata na Kamati ya Ujenzi WAMEFANIKIWA SANA kuhamasisha Wananchi wa Kata ya Bugoji kushiriki kwa hamasa kubwa kwenye MRADI huu unaotekelezwa kwa kasi kubwa.
KARIBU TUKAMILISHE Majengo ya “Dan Mapigano Memorial Secondary School” ili IFUNGULIWE na kuanza kutoa ELIMU ya SEKONDARI Januari 2020.