WANAVIJIJI NA MBUNGE WAO WA JIMBO WAAMUA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUHARAKISHA UJENZI WA HOSPITAL YA WILAYA YAO

Moja kati ya MAJENGO 7 ya Hospitali ya Wilaya yanayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti:

Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini WANAENDELEA kutoa SHUKRANI zao za dhati kwa SERIKALI yao kwa kutoa Tsh Bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya kwenye eneo lao.
Wananchi wa Vijiji 68 wa Jimbo la Musoma Vijijini, wakiongozwa na MADIWANI wao wa Kata 21, WAMEAMUA KUTOA MICHANGO ya FEDHA ili kushirikiana na SERIKALI yao kuharakisha ujenzi wa Hospitali yao ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) inayojengwa kwenye Kitongoji cha Kwikonero, Kijijini Suguti, Kata ya Suguti.
Kila KIJIJI kinachangia Tsh Milioni 2 kutoka kwenye Michango ya Fedha Taslimu na/au kutoka kwenye 20% ya Fedha zinazorejeshwa na Halmashauri yao kutoka kwenye Makusanyo ya Mapato yao ya ndani (own source).
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia kwa kutoa SARUJI MIFUKO 100 na amesema ataitoa wakati wo wote itakapohitajika.
MIUNDOMBINU ya AFYA ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
(1) Hospitali ya Wilaya: inajengwa
(2) Vituo vya Afya 2 (Murangi na Mugango)
(3) Zahanati:
 (a) Za Serikali: 24 zinatoa huduma
 (b) Za Binafsi: 4 zinatoa huduma
(4) Zahanati zinazojengwa Vijijini: 13 (NGUVUKAZI za Wanavijiji, Serikali, Mbunge wa Jimbo na Wadau wengine wa Maendeleo)
(5) Kituo cha Afya 1: kinajengwa Kijijini Nyambono (Wazaliwa wa Nyambono, Mbunge wa Jimbo na Wadau wengine wa Maendeleo)
ILANI YA UCHAGUZI YA CCM (2015-2020): Inatekelezwa kwa kasi kubwa – kila Kijiji kiwe na Zahanati moja, TUTAFIKA!
SHUKRANI KWA UONGOZI MZURI
DC wa Musoma, Dr Vicent Naano Anney  na DED, Ndugu John Kayombo WANAPONGEZWA SANA kwa Uongozi wao mzuri unaoleta MAFANIKIO makubwa kwenye UTEKELEZAJI wa Miradi ya Maendeleo kwenye Jimbo la Musoma Vijijini.