MWITONGO, BUTIAMA: KABURI (MAUSOLEUM) LA BABA WA TAIFA LINAPAKWA RANGI NA KUSAFISHWA

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ametekeleza KAZI aliyojipangia ya kila Mwaka kupaka rangi KABURI la Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere.

Prof Sospeter Mwijarubi Muhongo, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anaendelea KUTEKELEZA KAZI aliyojipangia ya kila Mwaka ya kupaka rangi KABURI la Baba wa Taifa, Hayati Mwl Julius Kambarage Nyerere. Kazi hii inafanywa kwa ushirikiano na Familia ya Baba wa Taifa.
Leo, Jumatano, 02.10.2019, Msaidizi wa Mbunge, Ndugu Fedson Masawa, amekabidhi rangi za kupaka KABURI (Mausoleum) la BABA wa TAIFA. Kazi zinaendelea hapo Mwitongo (angalia picha).
WANANCHI wanakaribishwa kwenye KUMBUKUMBUKU za BABA wa TAIFA nyumbani kwake Mwitongo, Butiama.
Ratiba inaonesha shughuli zitaanza tarehe 08.10.2019 na kufikia kilele chake tarehe 14.10.2019. Mashindano ya Mchezo wa Bao (Mchezo alioupenda sana Baba wa Taifa) yapo. Jimbo la Musoma Vijijini litawakilishwa na Kikundi 1 cha KWAYA na Kikundi 1 cha NGOMA za ASILI.
Mgeni Rasmi ni Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe Jaji Sinde Warioba. Viongozi wengine waliofanya kazi kwa karibu sana sana na Baba wa Taifa watakuwepo. KARIBUNI.