MATUMIZI YA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO YAJADILIWA HADHARANI

KIKAO cha KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO cha Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo kilichofanyika Kijijini Busamba, Kata ya Etaro.

 Jumanne, 17.09.2019, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, ALIITISHA KIKAO kwenye Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro KUJADILI na KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO.
Mbunge wa Jimbo hilo AMEWEKA UTARATIBU wa kufanya VIKAO vya pamoja vya Wananchi na Viongozi wao wa Serikali na Vyama vya Siasa wa ngazi mbalimbali WAKATI WA KUGAWA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO. Vikao hivyo vinafanywa kwa mzunguko ndani ya Kata 21 ya Jimbo hilo. Safari hii KIKAO kimefanyika kwenye KATA YA ETARO.
Wananchi na Viongozi wao wa Kata ya Etaro yenye Vijiji 4 walishiriki.
MADIWANI wa Vyama vyote vya Siasa, yaani, CCM na CHADEMA walishiriki.
CCM iliwakilishwa na Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Musoma Vijijini wakiwemo, Mwenyekiti wa Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Katibu wa Wilaya, Ndugu Stephene Koyo. Viongozi wengine wa CCM na Jumuiya zake walikuwepo.
TAARIFA YA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO
*Fedha hizi ni za Serikali na zinatunzwa na Halmashauri yetu.
*MIUNDOMBINU YA ELIMU kwenye Shule za Msingi na Sekondari bado zinahitaji KUBORESHWA sana, kwa hiyo Fedha za Mfuko wa Jimbo ZITACHANGIA juhudi za WANANCHI za kuboresha MIUNDOMBINU ya ELIMU Jimboni mwetu.
*Fedha taslimu HAZITOLEWI kwa WALENGWA na badala yake WALENGWA wanapewa VIFAA VYA UJENZI VILIVYOOMBWA na kununuliwa na Halmashauri.
*Mwaka wa Fedha wa 2018/2019, Tsh 50.43M zilipokelewa kwenye MFUKO wa JIMBO. Fedha zilizobakia Mwaka 2017/2018  zilikuwa Tsh 4.23M. JUMLA: Tsh 54.66M
*Fedha za MFUKO wa JIMBO kwa Mwaka 2018/2019 (Tsh 54.66M) ZILITUMIKA KUNUNUA: (i) MABATI 931 na (ii) SARUJI MIFUKO 1,155. VIFAA hivyo viligawiwa mashuleni na kila KATA ilipata MGAO wake.
* Fedha zilizopokelewa kwa Mwaka wa Fedha wa  2019/2020 ni Tsh 52.43M. Zilizobakia Mwaka jana ni Tsh 1.46M. JUMLA: Tsh 53.89M
MGAO WA Tsh 53.89M
*Kipaumbele cha kwanza ni Sekondari 2 zitakazofunguliwa Januari 2020.
*Sekondari hizo ni Dan Mapigano Memorial Secondary School ya Kata ya Bugoji na Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara.
*Kata nyingine 19 nazo zimepata MGAO wa VIFAA VYA UJENZI kulingana na maombi yaliyowasilishwa.
FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO kwa Mwaka 2018/2019 (Tsh 53.89M) zitatumika kununua na kugawa jumla ya: (i) NONDO 200, (ii) MABATI 1,026, (iii) SARUJI MIFUKO 1,150 na (iv) Iwapo bei zitakuwa nzuri na fedha kusalia, fedha hizo zinunue vifaa vya ujenzi na kuendelea kuvigawa ipasavyo.