KIKUNDI KINGINE CHA NGOMA ZA ASILI KUTOKA MKOA WA MARA CHAENDA KUSHINDANA NJE YA MKOA WAO

Msaidiyi wa Mbunge, Ndugu Hamisa Gamba akimkabidhi TIKETI ZA USAFIRI Kiongozi wa LIRANDI, Ndugu Mtatiro Ijanja.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, AMECHANGIA USAFIRI wa Kikundi cha LIRANDI cha Kijiji cha Masinono, Kata ya Bugwema kwenda mashindanoni Tukuyu, Mkoani Mbeya.
MASHINDANO haya yanajulikana kwa jina la, “TULIA TRADITIONAL DANCES FESTIVAL”, yatafanyika TUKUYU Mjini, tarehe 26-28.09.2019.
Mashindano haya yanatayarishwa na Mhe Dkt Tulia Ackson, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kikundi cha LIRANDI cha Kata ya Bugwema ndicho kilichukua ushindi wa kwanza kwa Mashindano ya NANENANE ya Ngoma za Asili ya Jimbo la Musoma Vijijini yaliyofanyika tarehe 10.08.2019 Kijijini Suguti.
MKOA WA MARA UNAWAOMBEA SANA WAWAKILISHI WAO WARUDI NA USHINDI WA KWANZA
*EGUMBA (Jimbo la Butiama) ichukue ushindi wa kwanza (kimataifa) huko Dar Es Salaam
*LIRANDI (Jimbo la Musoma Vijijini) ichukue ushindi wa kwanza huko Tukuyu, Mbeya