BUSAMBARA SECONDARY SCHOOL – WANAVIJIJI WAKUBALIANA KUONGEZA KASI YA UJENZI

Ziara ya M/Kiti wa CCM wilaya Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo kwenye eneo la ujenzi wa Busambara Secondary School, Kijijini Kwikuba, Kata ya Busambara

Jimbo la Musoma Vijijini lenye Kata 21 na Vijiji 68 lina Sekondari za Kata/ Serikali 18 na za Binafsi 2.
Wanavijiji WAMEAMUA kujenga SEKONDARI MPYA 9 ili kupunguza umbali watembeao Wanafunzi na Walimu, na kupunguza msongamano madarasani.
Kata ya Busambara yenye Vijiji 3 (Maneke, Kwikuba na Mwiringo) inakaribia kukamilisha Awamu ya Kwanza ya ujenzi wa Sekondari ya Kata yao.
Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa umekamilika na kila Darasa lina Madawati 40.
Wanavijiji na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wanaishukuru sana Benki ya NMB kwa kuwapatia Madawati 80 na Viti 80.
Ujenzi wa Ofisi ya Mwalimu Mkuu na ya Walimu wengine  unakamilishwa.
Wananchi wa Vijiji 3 vya Kata hiyo WAMEGAWANA KAZI za Ujenzi wa Vyoo, Maabara na Nyumba ya Mwalimu Mkuu. Kazi zimeanza.
Jana, Jumatatu, 16.09.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya ya Musoma Vijijini, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika WALIKAGUA MAENDELEO YA UJENZI wa Sekondari ya Busambara.
Vilevile walitumia fursa hiyo kuongea na Wanavijiji wa Kata ya Busambara. Maswali yaliulizwa na kujibiwa.
FEDHA na VIFAA vya ujenzi wa Busambara Secondary School vimetoka: (i) Serikalini (TAMISEMI)  Tsh 37.5M, na Halmashauri, Tsh 2 M, (ii) Mbunge wa Jimbo-Saruji Mifuko 150 na Bando 8 za Mabati, (iii) Wazaliwa wa Kata ya Busambara (Afande Nyakulinga, Joseph Chikongowe na Advocate Said Chiguma), (iv) Michango ya Wanavijiji wa Tsh 15,000 kutoka kila Kaya, (v) Michango ya WADAU wengine wa Maendeleo.
UAMUZI WA WANAVIJIJI
*NGUVUKAZI kutoka Vijijini iongezeke
*Ujenzi wa Vyoo ukamilike kabla ya tarehe 30 Oktoba 2019
*Ujenzi wa MAABARA ukamilike kabla ya tarehe 30 Novemba 2019
*Ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu Mkuu ukamilike ifikapo tarehe 30 Disemba 2019
*Busambara Secondary School IFUNGULIWE na kuchukua WANAFUNZI wa FORM Januari 2020.