UJENZI WA DAN MAPIGANO MEMORIAL SECONDARY SCHOOL WAENDELEA VIZURI

Ziara ya Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo wakiwa eneo la ujenzi wa Dan Mapigano Memorial Secondary School, Kijijini Bugoji, Kata ya Bugoji.

 
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijijini, Prof Sospeter Muhongo akiambatana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya, Ndugu Nyabukika Bwire Nyabukika WAMEFANYA ZIARA Kijijini Bugoji KUKAGUA UJENZI wa Dan Mapigano Memorial Secondary School.
 
Serikali, Wanavijiji na Viongozi wao, Mbunge wa Jimbo, na Wadau wengine  wa Maendeleo ya Kata ya Bugoji WANACHANGIA UJENZI WA SEKONDARI hii.
 
NGUVUKAZI ya Wanavijiji wa Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugiji IMESAIDIA SANA kuharakisha ujenzi huu ulioanza Disemba 2018.
 
Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa  vitano (5) umekamilika na kila Chumba (Darasa) kina MADAWATI 40. Ofisi za Mwalimu Mkuu na Naibu wake zimekamilika.
 
Ujenzi wa Vyoo, Maabara na Nyumba ya Mwalimu Mkuu UMEANZA na unaendelea.
 
LENGO KUU: Dan Mapigano Memorial Secondary School ifunguliwe Januari 2020 na Wanafunzi wengi wa Form I watoke Vijiji vya Kaburabura, Kanderema na Bugoji (Kata ya Bugoji).