BOMBA LA MAJI SAFI NA SALAMA – MRADI WA MUGANGO-KIABAKARI-BUTIAMA

UWEKAJI wa SAINI za UTEKELEZAJI wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Maji la Mugango-Kiabakari- Butiama kwenye Viwanja vya Shule ya Msingi ya Nyamisisi, Kata ya Kukirango, Kiabakari, Wilaya ya Butiama

AHADI ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Dkt John Joseph Pombe Magufuli IMEANZA KUTEKELEZWA.
Mradi wa Bomba la Maji Safi na Salama la kutoka Ziwa Victoria (Mugango, Musoma Vijijini) hadi Wilaya ya Butiama (Kiabakari-Butiama) umeanza kutekelezwa kwa SERIKALI na MKANDARASI kuwekeana SAINI ya UTEKELEZAJI wa MRADI huu wenye Thamani ya US$ 30.69 million (Tshs 70 billion).
Maji kiasi cha LITA MILIONI 35 (35,000 cu.m.) yatazalishwa Kijijini Kwibara (Kata ya Mugango) na kusafirishwa na kusambazwa kwenye VIJIJI vya Jimbo la Musoma Vijijini (kwa kuanzia Vijiji vya Kata za Mugango na Tegeruka) na Vijiji vya Jimbo la Butiama. Mradi utakamilika ndani ya MIEZI 24.
Serikali iliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Prof Kitila Mkumbo. Mkoa uliongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe Adam Malima. Wakuu wa Wilaya za Musoma na Butiama, Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya 2 hizo, Madiwani na Viongozi wengine wa Chama na Serikali walihudhuria TUKIO hili muhimu kwa Mkoa wa Mara.
Chief Japhet Wanzagi Nyerere, Mwenyekiti wa Bodi ya Maji Mkoa alihudhuria sherehe hizi.
Wabunge waliohudhuria ni Mhe Agnes Marwa, Mhe Amina Makilagi na Prof Sospeter Muhongo.
Wananchi na Viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya za Musoma na Butiama WANATOA SHUKRANI nyingi sana Mhe Rais Dkt John Joseph Pombe Magufuli na Viongozi wengine wote wa Serikali kwa KUKAMILISHA TARATIBU za UTEKELEZAJI wa Mradi huu.