WANAFUNZI WA NYAMBONO SECONDARY SCHOOL WAFURAHIA MADAWATI YALIYOTOLEWA NA BENKI YA NMB

baadhi ya Wanafunzi, Walimu na Viongozi wa Kata ya Nyambono na Kijiji cha Saragana WAKIPOKEA MSAADA WA Benki ya NMB wa Madawati 50 na Viti 50. Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo ALIWAKABIDHI Msaada huo wa Benki ya NMB.

Wanafunzi na Walimu wa Nyambono Secondary School iliyoko Kijijini Saragana, Kata ya Nyambono WANASHUKURU SANA SANA kwa MSAADA uliotolewa na Benki ya NMB wa MADAWATI 80 na VITI 80. Jana (07.08.2019), Shule iliyopokea Madawati 50 na Viti 50. Mengine yatapelekwa hivi karibuni.
Busambara Secondary School ya Kata ya Busambara itakayoanza kutoa Elimu ya Sekondari kuanzia Januari 2020 nayo IMEPOKEA MSAADA wa BENKI ya NMB wa MADAWATI na VITI ya idadi sawa na Nyambono Secondary School na kwa utaratibu huo huo.
WAZAZI na VIONGOZI wa Serikali na Chama (CCM) wa ngazi mbalimbali wa Kata ya Nyambono na Kijiji cha Saragana WAMETUMA SALAMU ZAO ZA SHUKRANI kwa BENKI YA NMB kupitia kwa Mbunge wao wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo.
Mwalimu Mkuu wa Nyambono Secondary School, Mwl Michael Mpasi, aliyekuwa mwenye furaha nyingi sana, amesema yeye mwenyewe ATATUMA SHUKRANI za KIPEKEE kwenye Benki ya NMB.
SHEREHE ZA UWEKAJI SAINI wa MRADI MKUBWA wa MAJI wa MUGANGO-KIABAKARI-BUTIAMA (BOMBA JIPYA LA MAJI)
Wananchi wanakaribishwa KUSHUHUDIA uwekaji SAINI kati ya SERIKALI na MKANDARASI wa UTEKELEZAJI wa Mradi huu. Gharama za Mradi ni US$ 30.69 (Takribani Tshs 70 bilioni).
Tukio hilo muhimu na kubwa litafanyika Kijijini Mugango (Mitambo ya Maji), tarehe 15.08.2019, saa 3 Asubuhi.
SHEREHE hiyo itatumbuizwa na KWAYA ya JIMBO na NGOMA ASILI ya JIMBO.
Vikundi hivi (Ngoma na Kwaya) vya Jimbo vitapatikana kwenye MASHINDANO ya NANENANE yatakayofanyika Jumamosi, 10.08.2019 kwenye Viwanja vya S/M Suguti, Kijijini Suguti.
Kata ipi itaibuka Mshindi wa Kwanza (Kikombe & Tsh Milioni 1) ya Ngoma za Asili? NGOMA ya Jimbo?
Kata ipi itaibuka Mshindi wa Kwanza (Kikombe & Tsh Milioni 1) wa KWAYA? KWAYA ya Jimbo?