*IDADI YA SHULE ZA MSINGI
Jimbo lina Jumla ya Shule za Msingi 111 za Serikali na 3 za Binafsi
Wananchi, Madiwani na Viongozi wao wengine, kwa kushirikiana na SERIKALI na Mbunge wao wa Jimbo wanajenga SHULE SHIKIZI mpya 10. Shule hizi hapo baadae zitapanuliwa na kuwa Shule za Msingi kamili zenye Darasa la I hadi VII.
* IDADI YA SHULE ZA SEKONDARI
Jimbo lina Jumla ya Sekondari 18 za Serikali na 2 za Binafsi.
Wananchi, Madiwani na Viongozi wao wengine, kwa kushirikiana na Serikali na Mbunge wao wa Jimbo wanajenga Sekondari mpya 8.
UAMUZI WA KUONGEZA HIGH SCHOOLS JIMBONI
Jimbo hili lina High Schools 2 tu, yaani Kasoma High School (Serikali) yenye MASOMO ya ARTS tu, na Nyegina High School (Binafsi, Katoliki) yenye MASOMO ya SAYANSI na ARTS.
MAPENDEKEZO YA KUONGEZA HIGH SCHOOLS ZA SERIKALI
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo amefanya VIKAO na Wananchi na Viongozi mbalimbali AKIWASHAWISHI kuboresha MIUNDOMBINU (k.m. Maabara, Ujenzi wa Mabweni) ya baadhi ya Sekondari zetu ili ZIPANULIWE na kuanza kutoa Elimu ya Kidato cha V na VI ya Masomo ya Sayansi.
Mapendekezo haya yanaungwa mkono na Wananchi na Viongozi wao wa ngazi mbalimbali wakiwemo MAAFISA ELIMU wa Halmashauri yetu.
Sekondari za BUGWEMA, MTIRO, MUGANGO na MKIRIRA ndizo ziko juu kwenye orodha ya kuweza KUANZISHA HIGH SCHOOLS za Masomo ya Sayansi. Sekondari nyingine nazo zina nafasi sawa na hizo iwapo Miundombinu ya Elimu ya kuanza High Schools itakuwepo. Kwa hiyo, kinachotakiwa ni KUWEKA MIUNDOMBINU INAYOHITAJIKA kukidhi MATAKWA ya uwepo wa High Schools.
Wananchi, MADIWANI, Mbunge wa Jimbo kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri, Ndugu John Kayombo na Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney WATATEKELEZA MRADI huu wa Ongezeko la High Schools za Serikali kwenye Jimbo letu.
Njia ya pili ya kuongeza High Schools Jimboni mwetu ni kukaribisha uanzishwaji wa High Schools za Binafsi (Private High Schools).
Mbunge wa Jimbo amefanya KIKAO na BODI ya Secondary ya Nyegina (Binafsi, Katoliki) na KUKUBALIANA kuimarisha na kuboresha High School yao. Mipango ya Utekelezaji inatayarishwa ili KUONGEZA IDADI ya Wanafunzi wanaosoma Masomo ya Sayansi ya Kidato cha V na VII Shuleni hapo.
Mbunge wa Jimbo hakuweza kufanya Kikao na BODI ya Bwasi Secondary School baada ya Shule hiyo kupata msiba. Kikao hicho kitafanyika baadae. Uongozi wa Bwasi Secondary School UNAKUBALIANA NA pendekezo la KUANZISHA High School yenye Masomo ya Sayansi.
MRADI WA KUBORESHA ELIMU YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZETU
Mbunge wa Jimbo amefanya VIKAO 2, kimoja (06.08.2019) na BODI ya Nyegina Secondary School, na kingine (07.08.2019) na AFISA ELIMU (DEOs) na Viongozi wengine wa Idara ya Elimu ya Halmashauri yetu kuhusu suala hili.
IMEKUBALIWA kwamba MRADI uanzishwe kwa UTEKELEZAJI wa pendekezo hili na Kituo cha Utekelezaji kiwe Kijijini Nyegina kwenye Madaraka Nyerere Library and Community Resource Center. Idara ya Elimu ya Halmashauri yetu na Mbunge wa Jimbo watashiriki kwenye Mradi huu. Wataalamu wa Elimu wanatayarisha MIPANGO ya UTEKELEZAJI wake.
KWA NINI TUNASISITIZA KUBORESHA ELIMU YA SAYANSI?
*Taifa litakalokuwa na UBUNIFU (INNOVATION) mkubwa kwenye TEKNOLOJIA na SAYANSI ndilo LITATAWALA UCHUMI wa Dunia yetu kwenye Karne hii na zijazo. Wenzetu wameingia kwenye “4th Industrial Revolution” ambayo imejikita kwenye Cyber Space, Digital Codes, Internet of Things (IoT), Artificial Intelligence (AI), Robotics, Genetic Engineering, Nanotechnologies, n.k. Africa isiachwe nyuma sana, nasi tupate Wanasayansi Mahiri.