WAFUGAJI WAAMUA KUTUMIA MIFUGO YAO KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI MPYA, ZAHANATI NA VYUMBA VYA MADARASA KWENYE SHULE YA MSINGI

HARAMBEE ya WANAKIJIJI na Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo ya ujenzi wa Nyasaungu Secondary School na Zahanati

Wakazi wengi wa Kijiji cha Nyasaungu ni WAFUGAJI. Kijiji hiki kiko ndani ya Kata ya Ifulifu, Musoma Vijijini.
Kata ya Ifulifuli haina Sekondari ya Kata. Watoto wa Kata hii wanatembea umbali usiopungua kilomita 3 kwenda kwenye Sekondari za Kata jirani – Mugango na Nyakatende Secondary Schools.
Kwa kuzingatia JIOGRAFIA (k.m. mito na mabonde) ya Kata ya Ifulifu, Wakazi wa Vijiji vya Kabegi na Kiemba (Kata ya Ifulifu) wanajenga Sekondari yao. Wakazi wa Kijiji cha Nyasaungu (Kata ya Ifulifu) nao wanajenga Sekondari yao.
MTINDO WA UCHANGIAJI WA KIJIJI CHA NYASAUNGU
Wanakijiji wa Kijiji hiki WAMEKUBALIANA kwamba MICHANGO yao kwenye MIRADI ya Maendeleo ITAZINGATIA WINGI  WA MIFUGO aliyonayo mchangiaji. Kwa MFANO kwenye kila awamu ya MCHANGO wenye NG’OMBE ZAIDI ya 51, wanachangia Tsh 200,000 (laki 2).
Kutokana na UTARATIBU huo wa uchangiaji, Kijiji kina MIRADI 3 inayotekelezwa kwa wakati mmoja – (i) Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji, (ii) Ujenzi wa Vyumba 2 vya Madarasa kwenye Shule ya Msingi Nyasaungu na (iii) Ujenzi wa Sekondari yao.
HARAMBEE ZA MBUNGE WA JIMBO
Leo, Jumatatu, 05.08.2019, Mbunge wa Jimbo Prof Sospeter Muhongo AMEPIGA HARAMBEE 2 Kijijini Nyasaungu na matokeo ni haya:
(i) HARAMBEE ya Ujenzi wa Nyasaungu Secondary School.
SARUJI:
*Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia SARUJI MIFUKO 67
*Mbunge wa Jimbo amechangia SARUJI MIFUKO 35
NONDO
*Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia NONDO 27
* Mbunge wa Jimbo amechangia NONDO 20
(ii) HARAMBEE ya Ujenzi wa Zahanati
*Mbunge wa Jimbo alishachangia SARUJI MIFUKO 100
*Leo, 05.08.2019, Wanakijiji na Viongozi wao wamechangia NONDO 20
*Leo, 05.08.2019, Mbunge wa Jimbo amechangia NONDO 20.