SEKONDARI MOJA YA KATA HAITOSHI – WANANCHI WAAMUA KUJENGA SEKONDARI YA PILI

Kikao cha Mbunge Prof Sospeter Muhongo na WANAVIJIJI kwenye eneo la ujenzi wa Sekondari MPYA ya PILI ya Kata ya Nyakatende

NYAKATENDE SECONDARY SCHOOL iliyo kwenye Kata ya Nyakatende inahudumia Kata 2 – Kata ya Nyakatende (Vijiji 4) na Kata ya Ifulifu (Vijiji 3). Kwa hiyo MSONGAMANO MADARASANI ni mkubwa.
Kata ya IFULIFU isiyokuwa na Sekondari, IMEAMUA kujenga Sekondari 2 kwa wakati mmoja. Kijiji cha Nyasaungu kinajenga Sekondari yake na Vijiji vingine 2 (Kabegi na Kiemba) vinajenga Sekondari yao.
Mbali ya Kata ya Ifulifu kujenga Sekondari zake, bado masuala ya UMBALI na WINGI wa Wanafunzi ndani ya Kata ya NYAKATENDE,  vimelazimisha Wananchi wa Kata hiyo KUAMUA kujenga Sekondari ya pili.
SEKONDARI MPYA ya Kata ya Nyakatende inajengwa kwenye Kijiji cha KIGERA ETUMA. Sekondari hii inajengwa na Vijiji 2 – Kigera Etuma na Kakisheri
MAENDELEO YA UJENZI
MABOMA ya Vyumba 2 vya Madarasa yamefikia hatua ya kuezekwa na MATOFALI ya kutosha ujenzi wa JENGO LA UTAWALA yapo tayari.
MICHANGO YA WANANCHI
Wananchi WAMEKUBALIANA kila mwenye umri wa kuanzia MIAKA 18 achangie TOFALI MOJA. Mawe, kokoto, mchanga na maji vinasombwa kwa zamu, Kitongoji kwa Kitongoji.
WADAU WANAOCHANGIA UJENZI HUU
Mbali ya MICHANGO ya thamani ya TOFALI MOJA ya Wanavijiji wenyewe, WAVUVI na WACHIMBAJI Wadogo Wadogo nao wanachangia ujenzi huu.
MICHANGO YA WAZALIWA WA VIJIJI VYA KIGERA ETUMA NA KAKISHERI
Hawa ni WADAU WAKUU wa Mradi huu na kwa sasa wafuatao wameunda KIKUNDI kwa ajili ya kuchangia ujenzi huu:
(1) Nyakiriga Kabende-Mwenyekiti
(2) Albinus Makanyaga-Mhasibu
(3)Joseph Mnibhi – Katibu
(4) Augostino Eugene
(5) Joseph Surusi
(6) Wambura Mujungu
(7) Marere Eugene
(8) Mareges Eugene
(9) Emmanuel Ekama
(10) Mareges Jela
(11) Kisha Charamba
(12) Garani Magafu
(13) Mugini Kibusi Marere
(14) Ngajeni Manumbu
(15) Lucas Mashauri
(16) Mutandu Kabende
(17) Boniphace Kitende
(18) Boniphace Changanya
HARAMBEE YA MBUNGE
Leo, Ijumaa, 02.08.2019, Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMEENDESHA HARAMBEE YA UJENZI wa Sekondarii hii MPYA inayojengwa Kijijini Kigera Etuma.
HARAMBEE imefanikisha kupata:
(i) Fedha: 324,000/= kutoka Wanavijiji waliokuwepo
(ii) SARUJI MIFUKO 68 kutoka kwa Wanavijiji waliokuwepo
(iii) SARUJI MIFUKO 100 kutoka kwa Mbunge Prof Sospeter Muhongo
UJENZI UNAENDELEA KWA KASI KUBWA – KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI MPYA INAYOJENGWA NA VIJIJI VIWILI.