UKARABATI WA MABWENI YA SEKONDARI YA BWASI

Ukarabati na Uboreshaji wa Mabweni ya Bwasi Secondary School (private, SDA) iliyoko Kijijini Bwasi, Kata ya Bwasi.

Jumatatu, 29.07.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Shule ya Sekondari Bwasi ni moja ya Sekondari mbili za Binafsi (private) zilizopo kwenye Jimbo la Musoma Vijijini. Nyingine ni Nyegina Secondary School inayomilikiwa na Kanisa Katoliki.
Bwasi Secondary School INAMILIKIWA na Kanisa la Waadventista Wasabato na ipo kwenye Kijiji cha Bwasi. Ilianzishwa Mwaka 1987.
Matokeo ya Mitihani ya Mwaka jana (2018) ya Form IV yalikuwa ya KURIDHISHA: Division I walifaulu wawili (2), Division II kumi (10), Division III ishirini (20) na Division IV wanne (4).
MAABARA
Bwasi Secondary School ina MAABARA zote tatu, yaani za Physics, Chemistry na Biology. Maabara hizi zinahitaji UBORESHWAJI mkubwa.
MABWENI:
Kwa sasa ukarabati unaendelea kwenye MABWENI 2 yote yenye uwezo wa kuchukua WANAFUNZI 140 –  moja la Wasichana na jingine la Wavulana. Bado kuna upungufu wa BWENI MOJA la Wasichana.
Mkuu wa Sekondari hii, Mwalimu Ibrahim Chacha amesema kwamba Miundombinu ya Shule hiyo haijakarabatiwa kwa muda mrefu, kwa hiyo sasa Shule imeamua kufanya ukarabati na UBORESHAJI wa Miundombinu hiyo ili KUBORESHA MAZINGIRA ya Utoaji na Upokeaji/Upataji wa Elimu bora.
Mwalimu Mkuu huyo anawashukuru Wadau wa Elimu walioguswa na kuhamasika katika uchangiaji wa kukamilisha kazi hii.
Wanafunzi wa Sekondari hii  wamefurahishwa na ukarabati wa MABWENI yao na wamehaidi kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri zaidi.
HARAMBEE iliyofanyika kwenye Mahafali ya Kidato cha IV (2018) iliwezesha Shule kuanza ukarabati wa Mabweni hayo mawili. Baadhi ya WALIOCHANGIA siku hiyo ni: (1) Prof Lawrence Museru, (2) Dr Freddy Jirabi Gamba, (3) Ndugu Misana Gamba, (4) Ndugu Shauri Makota, (5) Mara Conference of Seventh Day Adventist Church na (6) Watumishi wa Sekondari hiyo.
Mbunge wa Jimbo Profesa Sospeter Muhongo akishagawa VITABU vya SEKONDARI mara mbili kwenye Shule hiyo na kwenye HARAMBEE hiyo alichangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ukarabati wa Bweni la Wasichana.
Tarehe 05.08.2019, Mbunge huyo atafanya KIKAO na BODI ya Sekondari hii AKIWA na LENGO la KUWASHAWISHI kuanzisha BWASI HIGH SCHOOL yenye MASOMO ya SAYANSI.