HALMASHAURI YASHIRIKIANA NA MRADI WA BMZ (Ujerumani) KUTOA HUDUMA KWA VITUO VYA ELIMU YA WATOTO WENYE ULEMAVU 

Wanafunzi wenye ULEMAVU wakiwa masomoni, baada ya kupata Kifungua Kinywa (breakfast) Shuleni kwao, S/M Nyambono B, Kijijini Saragana, Kata ya Nyambono.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Vituo vya Elimu ya Wanafunzi wenye ULEMAVU ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini vimeanza kuhudumiwa na Halmashauri yao kwenye Kata za Nyambono, Mugango na Nyegina.
Vituo hivi vya Elimu vinajumuisha WATOTO wenye ULEMAVU wa Akili, Bubu, Viwete, Viziwi,  Vipofu na Wagonjwa wa Ngozi (Albino).
Kwenye Kata ya  Nyambono, Wanafunzi 20 wenye Ulemavu wanapata ELIMU ya MSINGI kwenye S/M Nyambono B, Kijijini Saragana.
Mwalimu Mkuu wa S/M Nyambono B, Mwl Abel Paul ambae pia ni Mwalimu anaefundisha Watoto wenye Ulemavu na Uhitaji wa Elimu Maalum, amesema ELIMU MAALUM hiyo ilianza kutolewa hapo Shuleni Mwaka 2017, baada ya kufanikiwa  kuwatafuta majumbani na kuwaleta Shuleni Watoto wenye Ulemavu.
Mwalimu Mkuu huyo amesema Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (yenye Jimbo la Musoma Vijijini) imekuwa ikitoa Fedha zinazosaidia Wanafunzi hao kupata Kifungua Kinywa (breakfast) wafikapo Shuleni asubuhi.
MRADI wa BMZ (Ujerumani) unatoa VIFAA MBALIMBALI vinavyohitajika kwa WANAFUNZI hao kama vile,  baiskeli, miwani ya kusomea, madaftari, kalamu, mabegi, n.k.
WANAFUNZI wenye ULEMAVU wanashukuru HALMASHAURI yao na MRADI wa  BMZ wa UJERUMANI kwa MISAADA yao inayowawezesha kupata Elimu.
Baadhi ya Wanafunzi wenye Ulemavu wa S/M Nyambono B wanakiri na kusema: “Mimi Magesa Adonias nimepewa Baiskeli ya kutembelea inayomwezesha kufika Shuleni, na baadae napenda kuwa Mwalimu” – alijieleza kwa Kiingereza chenye ufasaha mzuri.
Mwl Abel ameomba WADAU wa Maendeleo kuchangia ujenzi wa Vyumba vya Madarasa kwa ajili ya Matumizi ya Wanafunzi hao wenye Ulemavu hapo Shuleni.
Mbunge wa Jimbo Prof Muhongo amepokea ombi la Shule hiyo na AMEKUBALI KUCHANGIA ujenzi wa Vyumba vya Madarasa ya WANAFUNZI wenye ULEMAVU – KARIBUNI TUCHANGIE!