MRADI WA USAMBAZAJI WA MAJI  WATEKELEZWA KWENYE VIJIJI VITANO (5)

Utekelezaji wa MRADI wa USAMBAZAJI MAJI kwenye Vijiji vya Busungu, Bukima na Kwikerege.

Jumapili, 07.07.2019
Jimbo la Musoma Vijijini
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
MRADI wa USAMBAZAJI WA MAJI kwenye Vijiji vitano (5) umegawanywa kwenye Makundi mawili (2 LOTS) ili kuharakisha UTEKELEZAJI wake.
KUNDI I (Lot I)
Bulinga-Bujaga: Maji yatachukuliwa kutoka Kijijini Bujaga kwa ajili ya kusambaza kwenye Vijiji vya Bujaga na Bulinga, vyote vya Kata ya Bulinga. Mradi huu unatekelezwa na Mkandarasi MEDES COMPANY Ltd na gharama yake ni  Tsh.1,812,675,036 (Tsh 1.81 bilioni).
MRADI huo ulizinduliwa wakati wa Mbio za Mwenge kwenye Jimbo la Musoma Vijijini, tarehe 31.05.2019.
KUNDI II (Lot II)
Busungu-Bukima-Kwikerege: Maji yatachukuliwa kutoka Kijiji cha Bujaga na kusambazwa Vijijini Busungu (Kata ya Bulinga), Bukima (Kata ya Bukima) na Kwikerege (Kata ya Rusoli)
UTEKELEZAJI wa Mradi wa Usambazaji wa MAJI kwenye Vijiji hivyo vitano (5) unaendelea kwa kasi ya kuridhisha.
MRADI wa Busungu-Bukima-Kwikerege: unagharimu Tsh 1, 022, 531, 876 (Tsh 1.02 bilioni), unatekelezwa na Mkandarasi EDM NETWORK LTD JV FAU CONSTRUCTION LTD.
Kazi zinazotekelezwa ni pamoja na:
(i) Ujenzi wa Tenki lenye ujazo wa LITA 225,000, (ii) Ofisi ya Mradi, (iii) Vituo 18 vya kuchotea Maji, (iv) Viosk 2 vya kuuzia Maji, (v) Birika za kunyweshea MIFUGO na (vi) Utandazaji wa MABOMBA ya kusambaza MAJI.
Mkandarasi anayesimamia Mradi huu, Injinia Bosco Victor Sechu anasema kuwa hadi sasa wamejenga Vituo 18 vya maji, Ofisi, Viosk na Birika za kunyweshea MIFUGO. MRADI  unatekelezwa kwa muda wa MWAKA MMOJA na utakamilika ifikapo Septemba 2019.
Ndugu Charles Ndagile, Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Busungu ameeleza kwamba WANANCHI wa Eneo la MRADI wameupokea vizuri Mradi huu na KUKUBALI KUTOA MAENEO ya ARDHI yao ili kutandaza MABOMBA bila kudai fidia yo yote.
Aidha kukamilika kwa MRADI huu kutaondoa UKOSEFU wa upatikanaji na MAJI safi na salama kwa hivyo Vijiji na  akina MAMA hawatatembea tena umbali mkubwa kwenda kuteka MAJI.
Taratibu za kumpata Mkandarasi wa Mradi wa Vijiji vya Bugunda, Bwasi, Chimati na Kome zimeanza.
Kwa niaba ya WANANCHI wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mbunge wa Jimbo, Profesa Sospeter Muhongo anaendelea KUISHUKURU SANA SERIKALI kwa juhudi zake za kuanzisha na kutekeleza MIRADI ya USAMBAZAJI wa MAJI Vijijini mwao.