KIKUNDI CHA NGUVUKAZI CHATOA MSAADA WA CHAKULA SHULENI

Kikundi cha NGUVUKAZI kikiwa na mavuno ya MAHINDI kutoka shambani mwao

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jumamosi, 29.06.2019
Kikundi cha NGUVUKAZI kilichopo Kijiji cha Buanga, Kata ya Rusoli kilianzishwa Mwaka jana (2018) wakiwa chini ya Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Jamii (PCI, Project Concern International) lililowapa MAFUNZO ya KILIMO Wanachama wa Kikundi hicho na baadae wakaanzisha KILIMO cha MAHINDI, VIAZI LISHE, na MPUNGA.
Afisa Kilimo wa Kata, Ndugu Sevas Ngova ameeleza kwamba Kikundi cha NGUVUKAZI kilipata MAFUNZO ya ZAO JIPYA JIMBONI la ALIZETI na baada ya MAFUNZO walianza na SHAMBA DARASA kwa kutumia Mbegu walizopewa na Mbunge wa Jimbo,
Profesa Sospeter Muhongo. Mavuno ya awali ya ALIZETI yalikuwa ya MAGUNIA 10. Mbegu nyingine walizopokea kutoka kwa Mbunge wao huyo ni za MTAMA, MIHOGO na UFUTA.
Ndugu Tore Masamaki, Mwenyekiti wa Kikundi cha NGUVUKAZI ameeleza kwamba Kikundi hicho kilianza na WANACHAMA 18 na baada ya MAFANIKIO ya kuridhisha kupatikana, Wanachama wameongezeka na kufikia 30 (thelathini).
Kikundi cha NGUVUKAZI kinaendelea kushirikiana na Shirika la PCI ambalo moja ya malengo yake makuu ni kutoa CHAKULA mashuleni, ikiwemo Shule ya Msingi Bwenda.
“Kupitia Kikundi hiki mavuno yanayopatikana hupelekwa shuleni hapo, na mengine ni kwa manufaa yao wenyewe na familia zao – Ndugu Masamaki aliyasema haya na kuongeza kwamba sasa wanatafuta VIFAA vya UMWAGILIAJI waanze Kilimo hicho.
Mwalimu Mkuu wa S/M Bwenda, Mwl Christopher Cosmas  amekiri kupokea jumla ya KILO 220  za MAHINDI kutoka Kikundi cha NGUVUKAZI  kwa ajili ya CHAKULA cha WANAFUNZI.
Mwalimu Mkuu huyo anasema CHAKULA kinachotelewa kwa WANAFUNZI wote hapo Shuleni kimefanya UTORO usiwepo na HAMASA ya Wanafunzi kupenda kupata ELIMU imeongezeka.
Aidha Diwani wa Kata ya Rusoli, Mhe Boaz Nyeura ameshukuru Kikundi cha NGUVUKAZI kwa jitihada zake na kupitia vikao vya hadhara ameomba VIKUNDI vingine kujitokeza kusaidia UPATIKANAJI wa CHAKULA kwa Shule nyingine ndani ya Kata yao ya Rusoli.