WANANCHI WA KATA YA NYEGINA WAAMUA KUHARAKISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SEKONDARI YAO MPYA

Kata ya Nyegina yenye vijiji vitatu (Kurukerege, Mkirira na Nyegina) inazo sekondari mbili ambazo ni Mkirira na Bukwaya. Sekondari ya Bukwaya ni mpya, ilifunguliwa Julai 2022.

Uharakishaji wa ujenzi wa miundombinu ya Bukwaya Sekondari:
Sekondari hii ina mapungufu mengi na wanavijiji wa Kata ya Nyegina wameamua kuongeza kasi ya ujenzi wa miundombinu ya shule yao.

Uamuzi huo ulifanywa kwa kumshirikisha Mbunge wao, Prof Sospeter Muhongo alipotembelea shule hiyo siku ya Alhamisi, 28.3.2024

Tarehe 30.4.2024:
Ifikapo tarehe hii, vyumba viwili vya madarasa ambavyo tayari vimeezekwa vitakuwa vimekamilishwa. Mbunge wa Jimbo amewakabidhi Saruji Mifuko 150 iliyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo.

Tarehe 30.5. 2024:
Ifikapo tarehe hii, matundu sita (6) ya choo yatakuwa yamekamilika

Mwezi Julai 2024:
Mbunge wa Jimbo atapiga Harambee ya kuanza ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi, ambayo ni fizikia, kemia na bailojia.

Michango ya ujenzi wa Bukwaya Sekondari:
Sekondari hii alianza kujengwa kwa nguvu za wananchi na Mbunge wa Jimbo. Orodha ya michango yote imetunzwa shuleni hapo.

Serikali inashukuliwa sana kwa kuchangia Tsh Milioni 40 (arobaini) zikiwa ni fedha za UVIKO.

Picha za hapa inaonesha:
Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, na wananchi wa Kata ya Nyegina, wakiwemo walimu na wanafunzi wa Bukwaya Sekondari, na wanafunzi wa Shule ya Msingi Nyegina. Hii ilikuwa siku ya Alhamisi, 28.3.2024

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

P. O. Box 6
Musoma

Tarehe:
Jumatatu, 1.4.2024