MISIBA KISIWANI RUKUBA: DHORUBA KUBWA YAVUNJA MTUMBWI NA KUSABABISHA VIFO VITATU

Tunasikitika kupoteza ndugu zetu 3 waliokufa maji siku ya Jumapili usiku kuamkia Jumatatu (jana, 15.1.2024). Dhoruba kubwa ilivunja mbao za mtumbwi na maji yakazamisha mtumbwi huo.

Mtumbwi ulikuwa na wavuvi 4: mmoja amesalimika (kwao Musoma Mjini) na watatu wamekufa maji (2 kwao Maneke & 1 kwao Nyegina)

Utafutaji wa miili ya marehemu:
*Ajali ilitokea eneo la mbali kutoka Kisiwani Rukuba - mwendo wa takribani masaa matatu kuelekea Kisiwa cha Goziba (Bukoba)

*Mitumbwi 10 inaanza kazi ya kutafuta miili hiyo kesho. Mafuta yanayohitajika ni lita 500 au zaidi.

Michango ya mafuta ya kutafuta waliokufa maji
(i) Wana-Rukuba wamejichangia lita 300
(ii) Mbunge wa Jimbo amechangia lita 200

Maombi ya michango kutoka vyanzo vingine:
Mahitaji ya misiba hii mitatu ni mengi na makubwa. Tafadhali changia misiba hii kwa kutuma fedha kwenye Akaunti ya Kisiwa/Kijiji cha Rukuba.

Benki: NMB
Akaunti Na.: 30302300701
Jina la Akaunti: Serikali ya Kijiji cha Rukuba

Pichani:
Maombolezo yanaendelea pembeni mwa Ziwa Victoria, Kisiwani Rukuba.

Tunamwomba Mwenyezi Mungu awape nguvu na matumaini mema wanafamilia wa marehemu hao watatu. Tuendelee kuwafariji wafiwa!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 16.1.2024