SEKONDARI ILIYOFUNGULIWA MWAKA 2006 YAAMUA KUANZA KUJENGA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI

Nyanja Sekondari ni ya Kata ya Bwasi yenye vijiji vitatu (3) vyenye jumla ya vitongoji ishirini na vitatu (23). Vijiji hivyo ni Bugunda, Bwasi na Bugunda.

Sekondari hii ilifunguliwa Mwaka 2006, na kwa sasa ina jumla ya wanafunzi 547, na walimu 12 wenye ajira, na 5 wa kujitolea.

Harambee ya ujenzi wa maabara:
Sekondari haina maabara hata moja na mwitikio wa wanafunzi kusoma masomo ya sayansi ni mdogo sana

Kwa mfano, Kidato cha Nne (Form IV) chenye jumla ya wanafunzi 96, ni wanafunzi 13 tu wanaosoma somo la Fizikia.

*Jana, Jumatatu, 9.10.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini na Kamati ya Siasa ya Wilaya (CCM) waliendesha HARAMBEE ya kuanza ujenzi wa maabara za Fizikia, Kemia na Baiolojia za sekondari hiyo.

Mapato ya Harambee:
*Fedha: Tsh 1,105,000
*Saruji Mifuko 141
(ikiwemo Mifuko 100 ya Mbunge wa Jimbo)

Kamati ya Ujenzi:
Kamati ya Ujenzi ya watu wanne (4) imeundwa.

KARIBUNI TUCHANGIE UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA ZA MUSOMA VIJIJINI

Idadi ya Sekondari Jimboni (Kata 21) mwetu:
*25 za Kata
*2 za Binafsi
*5 zinajengwa

Pichani ni Harambee ya jana iliyofanyika Nyanja Sekondari, Kijijini Kome, Kata ya Bwasi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 10.10.2023