WANAVIJIJI WAAMUA KUJENGA MAABARA TATU NDANI YA MIEZI MITATU

matukio mbalimbali ya: *HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ya kuchangia ujenzi wa Maabara za Mtiro Sekondari. Harambee ilifanyika shuleni hapo. *Usombaji wa Saruji na Mchanga wa kuanzia ujenzi

Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wameamua kujenga Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari yao ya Kata, Mtiro Sekondari.

Kata ya Bukumi ina vijiji vinne ambavyo ni Buira, Bukumi, Buraga na Busekera.

TAKWIMU ZA MTIRO SEKONDARI
*ilifunguliwa Mwaka 2006
*idadi ya wanafunzi ni 682
*idadi ya walimu ni 17 (13 wenye ajira ya Serikali na 4 wa kujitolea)
*hakuna Maktaba
*hakuna Maabara hata moja ya Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 17 kati ya 110 wa Kidato cha Tatu (Form III), 15.5%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 25 kati ya 123 wa Kidato cha Nne (Form IV), 20.3%, ndio wanasoma Masomo ya Sayansi

*wanafunzi 5 kati ya 682 ndio wamechangia chakula cha mchana

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO
Alhamisi, 9.3.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo aliendesha HARAMBEE shuleni hapo kwa lengo la kupata fedha za ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi (Fizikia, Kemia & Baiolojia) za Mtiro Sekondari.

MATOKEO YA HARAMBEE
*Michango ya Wanavijiji iliongozwa na Diwani wao, Mhe Munubhi Musa. Wazaliwa wa Kata ya Bukumi nao wameanza kuchangia.

Fedha Taslimu:
Tsh 494,000
Fedha (ahadi)
Tsh 4,493,000
Saruji Mifuko 26
Mchanga Lori 5

*Michango ya Mbunge wa Jimbo, ameanza kwa kutoa:
Saruji Mifuko 150

UJENZI KUANZA JUMATATU, 13.3.2023
*Wanavijiji na Viongozi wao wa Kata ya Bukumi wameamua kuanza kutekeleza mradi huu mara moja.

*Mchanga wa kuanzia kazi tayari umesombwa

*Saruji Mifuko 75 kati ya 150 iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo tayari imefikishwa shuleni.

*Ifikapo Juni 2023, maabara 3 ziwe zimekamilika.

MAWASILIANO YA KUTOA MCHANGO WAKO
*Headmaster
Mtiro Sekondari
0758 487 478

WADAU wa MAENDELEO:
Wanavijiji wa Kata ya Bukumi wanaomba sana Wadau wa Maendeleo wajitokeze kuchangia utekelezaji wa mradi huu ambao ni muhimu sana kwa uboreshaji wa miundombinu ya elimu itolewayo Mtiro Sekondari - tunatanguliza shukrani zetu za dhati kwa wachangiaji wote.

Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini anaendelea na kampeni yake ya kuhamasisha na kuchangia ujenzi wa Maabara 3 za Masomo ya Sayansi kwenye Sekondari zote za Jimboni mwao.

Picha za hapa zinaonesha matukio mbalimbali ya:
*HARAMBEE ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini ya kuchangia ujenzi wa Maabara za Mtiro Sekondari. Harambee ilifanyika shuleni hapo.
*Usombaji wa Saruji na Mchanga wa kuanzia ujenzi

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumamosi, 11.3.2023