HARAMBEE YA UJENZI WA SEKONDARI MPYA KIJIJINI MUHOJI

Harambee ya ujenzi wa Muhoji Sekondari ya Kijijini Muhoji, Kata ya Bugwema.

Kijiji cha Muhoji ni moja kati ya vijiji vinne (4) vya Kata ya Bugwema - vingine ni Masinono, Kinyang'erere na Bugwema.

Kata hii ina Sekondari moja iitwayo Bugwema ambayo kwa sasa imeelemewa sana kwa sababu hizi:

*Kidato cha Kwanza (Form I) cha mwaka huu (2023) kina jumla ya WANAFUNZI 362 walioko kwenye Mikondo 7 ya wanafunzi 50 kwa kila mkondo. Iwapo kila mkondo ungalikuwa wa Wanafunzi 40, Form I hii ingalikuwa na Mikondo 9.

*Walimu 10 tu kwa Sekondari yenye jumla ya Wanafunzi 748.

Mbali ya mirundikano hiyo kwenye Bugwema Sekondari, bado wanafunzi wa kutoka Kijiji cha Muhoji wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita 24-30 kwenda na kurudu kutoka masomoni.

HARAMBEE YA MBUNGE WA JIMBO

Leo, Jumanne, 24.1.2023, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ameendesha HARAMBEE ya kuchangia ujenzi wa MUHOJI SEKONDARI.

MICHANGO ILIYOPATIKANA

(i) Wanakijijiji wakiongozwa na Diwani wa Kata, Mhe Clifford Machumu wamechangia:

*Saruji Mifuko 124
*Fedha taslimu, Tsh 305,000

Michango hiyo ya wananchi ni mbali na michango yao mingine ya:
*Nguvukazi - kusomba mawe, mchanga na kokoto.
*Tsh 45,000 kwa kila kaya

(ii) DC wa Wilaya ya Musoma, Mhe Dkt Halfan Haule amechangia:

*Saruji Mifuko 20
*Jana alishiriki kwenye ufyatuaji wa matofali

(iii) Mbunge wa Jimbo amechangia:
*Saruji Mifuko 150
*Ataendelea kuchangia

MALENGO YALIYOWEKWA;

*Ujenzi wa Vyumba 4 vya Madarasa vyenye Ofisi 2 (katikati) za Walimu na Choo chenye Matundu 8 ukamilike kabla ya 30 Julai 2023

*Muhoji Sekondari ifunguliwe Januari 2024

TUNAKUKARIBISHA kuchangia ujenzi wa Muhoji Sekondari. Mchango wako mpelekee:

Mtendaji wa Kijiji (VEO)
Samwel Mourice
0686 557 264
0769 458 012

ELIMU NI UCHUMI
ELIMU NI MAENDELEO

KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SHULE ZETU

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz

Tarehe:
Jumanne, 24.1.2023