WANAKIJIJI WA KITONGOJI CHA GOMORA WAJENGA SHULE MPYA KUONDOKANA NA ADHA WANAYOPATA WATOTO WAO YA KWENDA MBALI MASOMONI

Ujenzi unaoendelea wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu ya Shule Shikizi ya Kitongoji cha Gomora, Kijijini Musanja Kata ya Musanja

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini kwa sasa linajenga SHULE MPYA ZA MSINGI 12 (Shule Shikizi 12) ili kutatua matatizo sugu mawili ambayo ni:
*Umbali mrefu wanaotembea Wanafunzi kwenda masomoni (umbali wa zaidi ya kilomita 4)
*Mirundikano ya Wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa (Wanafunzi zaidi ya 45)
SHULE SHIKIZI 12 zinazojengwa ni: Binyago, Buanga, Buraga, Egenge, Gomora, Kaguru, Karusenyi, Kihunda, Mwikoko, Nyasaenge, Rwanga na Ziwa.
SHULE ZA MSINGI zilizopo ni:
*111 za Serikali
*3 za Binafsi
KITONGOJI CHA GOMORA
Kata ya Musanja ina Vijiji vitatu ambavyo ni Musanja, Nyabaengere na Mabui Merafuru.
WANAKIJIJI wa Kitongoji cha Gomora kilichopo Kijiji cha Musanja wameanza ujenzi wa shule mpya ili kuondokana na adha ya watoto wao kutembea umbali mrefu kwenda masomoni kwenye S/M MUSANJA.
MWALIMU MKUU, Mwl Ngasa Msabi ameeleza kuwa Kijiji cha Musanja kina Shule moja ya Msingi ambayo ni S/M MUSANJA iliyofunguliwa Mwaka 1956, kwa sasa ina:
*Wanafunzi 815
*Walimu 8, Pungufu 10
*Vyumba 7 vya Madarasa, Pungufu 12
WANAFUNZI wa  KITONGOJI cha GOMORA wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 4 kwenda masomoni kwenye S/M Musanja.
Wengine wanatembea umbali mrefu zaidi kwenda masomoni kwenye Shule za Msingi jirani za Lyasembe (Kata ya Murangi), na Bwenda  (Kata ya Rusoli).
MWENYEKITI wa Kitongoji cha Gomora, Ndugu Sospeter Mjarifu ameeleza kuwa WANAKIJIJI wa Kitongoji hicho wameamua kujenga shule yao kwa kutumia MICHANGO ya WANAKIJIJI, DIWANI wa KATA, MBUNGE wa JIMBO na WADAU wengine wa MAENDELEO.
HADI SASA MICHANGO imetolewa na:
*WANAKIJIJI:
(i) kuchimba msingi wa Vyumba vipya 2 vya Madarasa na Ofisi 1 ya Walimu
(ii) kusomba mawe, mchanga na maji ya ujenzi
(iii) kuchangia fedha taslimu, Tsh 15,000/= kutoka kila Kaya
*DIWANI WA KATA:
Ndugu Ernest Mwira alitayarisha HARAMBEE ambayo yeye na WADAU wa MAENDELEO wamechangia:
(i) Fedha Taslimu Tshs1.3 Milioni
(ii) Mifuko ya Saruji 63 na Nondo 8
*MBUNGE WA JIMBO:
Prof Sospeter Muhongo ameanza kuchangia ujenzi huu kwa kutoa SARUJI MIFUKO 50.
LENGO KUU LA WANAKIJIJI:
“Shule Shikizi Gomora ifunguliwe Januari 2022
OMBI kutoka Kitongoji cha Gomora ni kupata MICHANGO kutoka Halmashauri yetu na kutoka kwa Wadau wengine wa Maendeleo kukamilisha ujenzi wa SHULE SHIKIZI GOMORA.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini