KASI YAONGEZEKA KWENYE UTEKELEZAJI WA MIRADI YA USAMBAZAJI WA MAJI YA BOMBA KUTOKA ZIWA VIKTORIA

hatua mbalimbali zilizofikiwa kwenye  utekelezaji wa MRADI wa MAJI ya BOMBA kutoka Ziwa Viktoria ya VIJIJI vya Makojo na Chitare.

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
JIMBO la MUSOMA VIJIJINI lina KATA 21 zenye VIJIJI 68 na VITONGOJI 374
VIJIJI vyote 68 vina MIRADI ya MAJI ya BOMBA ya kutoka Ziwa Viktoria inayoendelea kutekelezwa kwa Mwaka huu wa Fedha (2020/2021) na Mwaka ujao (2021/2022).
FEDHA ZILIZOTUFIKIA HIVI KARIBUNI KUKAMILISHA BAADHI YA MIRADI
(1) Ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Suguti/Kusenyi
Tsh 84,000,000.
(2) Upanuzi wa Mradi wa Maji kutoka Suguti kwenda  Kwikonero, Rwanga na Kasoma
Tsh 80,000,000
(3) Mradi wa Maji wa Butata/Kastamu
Tsh 286,184,476
Jumla zimeletwa
Tsh 450,184,476
MRADI WA MAJI WA VIJIJI VYA CHITARE NA MAKOJO (Wanavijiji 10,178)
Mradi huu, kama ilivyo mingine unatekelezwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Maji (National Water Fund, NWF)
MENEJA wa RUWASA (W), Injinia Edward Sironga  amesema kwamba jumla ya gharama za Mradi huu ni Tsh 1,071,154,700.00/= (Tsh bilioni 1.07), na kwamba ulianza kutekelezwa Mwaka 2014. MKANDARASI ni Interelty Builders Ltd.
KIONGOZI huyo wa RUWASA ameelezea kuwa MRADI huo UMETEKELEZWA kwa ASILIMIA 90 (90%), na utakamilishwa kabla ya tarehe 30 Juni 2021.
KAZI ZILIZOKAMILIKA ni:
*Ujenzi wa Mitambo ya kusukuma Maji kutoka kwenye chanzo, na kuweka Mtandao wa Mabomba yenye urefu wa km 18.
*Ufungaji wa Mfumo wa Umeme
*Ujenzi wa Vitekea Maji (DP) 18
*Ujenzi wa Vioski 4
*Ujenzi wa Manteki 2 ya Maji
   (i) Tank 1: Lita 100,000
   (ii) Tank 2 Lita 75,000
DIWANI wa Viti Maalum wa Kata ya Makojo, Mhe Tabu Machumu amesema kukamilika kwa MRADI huu  kutaondoa matatizo ya upatikanaji wa MAJI kwenye VIJIJI vya Chitare na Makojo.
DIWANI huyo, kwa niaba ya WANAVIJIJI  watakaonufaika na MAJI hayo ya BOMBA, ametoa SHUKRANI nyingi kwa SERIKALI kwa uamuzi wake wakutoa fedha za ujenzi na ukamilishaji wake.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini