WANANCHI NA SERIKALI WASHIRIKIANA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA RUSOLI SEKONDARI

WANAVIJIJI na VIONGOZI wao (akiwemo Diwani wao Mhe Boaz Nyeura) washiriki kwenye ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa cha RUSOLI SEKONDARI

Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
RUSOLI SEKONDARI ni Shule ya Kata ya Rusoli iliyofunguliwa Mwaka 2010. Kata hii ina Vijiji 3 ambavyo ni: Buanga,  Kwikerege na Rusoli.
IDADI YA VYUMBA VYA MADARASA
MWALIMU MKUU wa Sekondari hii, Mwalimu Tausi Juma amesema kuwa Shule ina jumla ya WANAFUNZI 444. Mahitaji ya Vyumba vya Madarasa ni 12 vilivyopo ni 10.
Kutokana na Ufaulu wa Wanafunzi wa Kidato cha kwanza  kuongezeka, kuna MIRUNDIKANO mikubwa ya WANAFUNZI madarasani. Kwa mfano, KIDATO cha KWANZA chumba kimoja cha Darasa kina WANAFUNZI 54 badala ya 40!
MAABARA 3 (Fizikia, Kemia & Bailojia)
SEKONDARI hii inazo MAABARA zote tatu ambazo Vyumba vyake vimo ndani ya JENGO moja.
SERIKALI ilitoa Tsh MILIONI 20 kuboresha na kukamilisha Maabara ya Kemia, na hivi karibuni SERIKALI imetoa Tsh MILIONI 30 kuboresha na kukamilisha Maabara ya Fizikia.
UJENZI WA VYUMBA VIPYA VYA DARASA
MTENDAJI KATA ya Rusoli, Ndugu Goodluck Mazige amesema WANANCHI WAMEAMUA kujenga VYUMBA VIPYA 3 VYA MADARASA ili kuondoa MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani.
KIONGOZI huyo, na DIWANI wa Kata hiyo, Mhe Boaz Nyeura wamesema wanaanza na ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa ambacho kitakamilika kabla ya tarehe 30.5.2021
MICHANGO YA WANAVIJIJI
*NGUVUKAZI ya kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*Tsh 5,000 kuchangwa na kila KAYA ndani ya KATA hiyo ya Rusoli.
DIWANI Mhe Boaz Nyeura anaomba WADAU wa MAENDELEO wakiwemo WAZALIWA na Kata hiyo wajitokeze na kuchangia ujenzi wa Vyumba Vipya 3 vya Madarasa ya Sekondari yao.
DIWANI huyo anatoa SHUKRANI nyingi sana kwa wanaochangia UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya RUSOLI SEKONDARI ambao ni:
*WANAVIJIJI wa Kata yao
*SERIKALI yetu
*WAZALIWA wa Kata hiyo ambao ni: Profesa Mselu, William Makunja, Berias Mkama, Jeff Makongo, Laiton Samamba, Robert Masige, Majura Maingu, Feada Manyiri na Stephan Kaema.
*YEBHE CHIKOMESHE ni Kikundi cha WAZALIWA wa Kijiji cha Rusoli ambacho KINACHANGIA MAENDELEO ya kwao nyumbani yakiwemo ya Rusoli Sekondari. Kikundi hiki kimechimba KISIMA cha MAJI ya Kijijini kwao.
Vilevile, Kikundi hiki kilinunua VIFAA vya MAABARA vya Rusoli Sekondari na hivi karibuni kimenunua Computer na Photocopy ya Sekondari hiyo –  HONGERENI SANA SANA.
MICHANGO YA MBUNGE WA JIMBO
*Saruji Mifuko 70
*Kuchangia kulipa POSHO ya Mwalimu wa Kujitolea wa Masomo ya Sayansi kwa Mwaka mmoja.
*Vitabu vingi vya Maktaba
KARIBUNI TUCHANGIE MAENDELEO YA RUSOLI SEKONDARI
*MATOKEO ya KIDATO cha  II (2020)
Jumla ya Watahiniwa: 107
Div I = 6     Div II= 9
Div III = 26 Div IV= 66
*MATOKEO ya KIDATO cha IV (2020)
Jumla ya Watahiniwa: 64
Div = 1      Div II = 6
Div III = 7  Div IV = 44
Div O = 6
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or. tz