SEKONDARI MPYA ILIYOFUNGULIWA MWAKA HUU (2021) YAANZA UJENZI WA MADARASA MAPYA YATAKAYOHITAJIKA MWAKANI (2022)

ujenzi unaoendelea wa Vyumba vipya vya Madarasa vitakavyohitajika Mwakani (Januari 2022) kwenye SEKONDARI MPYA iliyofunguliwa Mwaka huu (tarehe 22.2.2021).

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KIGERA SEKONDARI ni Shule mpya iliyoanza ujenzi wake Mwaka 2019 kwa NGUVU za WANANCHI wa Vijiji 2 wakishirikiana na WADAU wa MAENDELEO (Wazaliwa wa Vijiji hivyo viwili) na VIONGOZI wao (Madiwani 2 kwa nyakati tofauti, na Mbunge wa Jimbo)
SEKONDARI hii ni ya Vijiji 2 vya Kakisheri na Kigera vyote vya Kata ya Nyakatende. Hii ni SEKONDARI ya PILI ya Kata hii. Sekondari yake ya KWANZA (Nyakatende Sekondari) iko Kijijini Nyakatende.
MIUNDOMBINU ILIYOKWISHAKAMILISHWA
*Vyumba Vipya 2 vya Madarasa vinavyotumiwa na Kidato cha Kwanza
*Choo chenye Matundu 11
*Jengo la Utawala lenye Ofisi 9
SHULE KUFUNGULIWA
KIGERA Sekondari ilifunguliwa rasmi tarehe 22.2.2021 na tayari WANAFUNZI 122 wa KIDATO cha KWANZA wameanza masomo shuleni hapo.
IDADI YA WALIMU
*SEKONDARI hii mpya ina WALIMU 5 wa kuajiriwa na MWALIMU 1 wa kujitolea.
UJENZI UNAONDELEA
*Nyumba ya Mwalimu (inakamilishwa)
*Maabara 3 (zinakamilishwa)
WACHANGIAJI WA AWAMU YA KWANZA YA UJENZI (2019-2021):
*WANAVIJIJI – Nguvukazi (kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji)
*WANAVIJIJI – Fedha taslimu Shilingi 2,000 kwa kila Mkazi (ndani ya Vijiji hivyo viwili) mwenye umri wa zaidi ya Miaka 18
*WAZALIWA wa Vijiji 2 – kulipa gharama za Mafundi
*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo
^Saruji Mifuko 150
^Mabati 108
*MBUNGE huyo wa JIMBO amelipia PANGO la miezi 6 (Februari – Julai 2021) ili WALIMU 2 wapate makazi Kijijini Kigera karibu na Sekondari hiyo.
*MFUKO wa JIMBO
^Saruji Mifuko 300
^Mabati 216
*HALMASHAURI
(Musoma DC)
 ^Tsh Milioni 5
MADAWATI NA SAMANI ZA OFISI ZA WALIMU
*WAZAZI wa WANAFUNZI 122 wa Kidato cha kwanza
^Madawati
*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere Kisha
^Samani za Ofisi za Walimu (Viti 8 na Meza 4)
MAJI YA BOMBA
*RUWASA WILAYA inakamilisha ujenzi wa Miundombinu ya MAJI ya BOMBA (kutoka Ziwa Victoria) ya Sekondari hii.
UJENZI WA VYUMBA VIPYA 3 VYA MADARASA YA MWAKANI (2022)
MAOTEO ya WANAFUNZI wa KIDATO cha KWANZA wa Mwakani (2022) ni kupokea WANAFUNZI kati ya 132 na 150 kwenye Sekondari hii.
Kwa hiyo, vinahitajika VYUMBA (vingine) VIPYA 3 vya Madarasa.
UJENZI WA AWAMU YA PILI (kuanzia April 2021 na kuendelea)
WANAVIJIJI wenye Sekondari hii (Vijiji 2 – Kakisheri & Kigera) WAMEANZA ujenzi wa VYUMBA hivyo 3 vitakavyohitajika mwakani (Januari 2022) na BOMA la CHUMBA kipya cha kwanza litakamilika kabla ya tarehe 30.4.2021.
Ujenzi utaendelea na kuhakikisha ifikapo Septemba 2021, MABOMA mengine mawili (2) yatakuwa yamekamilishwa.
WACHANGIAJI WA UJENZI WA AWAMU YA PILI
*WANAVIJIJI wa Vijiji 2 wanaendelea kujitolea (NGUVUKAZI) kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.
*WANAVIJIJI hao wanachangia fedha taslimu Shilingi 1,000 kwa kila mwenye umri wa zaidi ya miaka 18.
*MZALIWA wa Kijiji cha Kigera, Ndugu Lucas Mashauri – ameanza kuchangia ujenzi huu mpya kwa kutoa Saruji Mifuko 10.
*Ndugu Lucas Mashauri ni MCHANGIAJI MKUU wa Miradi ya Maendeleo ya Kata ya kwao ya Nyakatende – HONGERA SANA NDUGU YETU!
TUNAKARIBISHWA KUCHANGIA UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA KIGERA
Mwenyekiti wa Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura anaendelea KUWAKARABISHA WADAU wa MAENDELEO kuchangia ujenzi huu unaoenda kwa KASI kubwa na UBORA wa juu.
Aidha, MWENYEKITI huyo anatoa shukrani za dhati kwa WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji vya Kakisheri na Kigera, DIWANI na MBUNGE wao kwa MICHANGO yao kwenye Mradi huu wa Maendeleo ya Wananchi wa Kata ya Nyakatende.
SHUKRANI za kipekee wanapewa Mkuu wa Wilaya (DC), Dr Vicent Naano Anney na Mkurugenzi (DED), Ndugu John Kayombo kwa usimamiaji mzuri na makini wa ujenzi wa KIGERA SEKONDARI.
Hii ni KIGERA SEKONDARI inayojengwa na WANANCHI wa Vijiji 2 vya Kakisheri na Kigera vyote vya Kata ya Nyakatende ambayo sasa inazo SEKONDARI MBILI (2) za Kata.
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini