WANAVIJIJI WASHIRIKIANA NA SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU – KITONGOJI CHAJENGA SHULE SHIKIZI

Miundombinu ya SHULE SHIKIZI EGENGE inayojengwa ndani ya Kitongoji cha Egenge, Kijiji cha Busamba, Kata ya Etaro.

 

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

JIMBO la MUSOMA laendelea kushirikiana na SERIKALI kutatua MATATIZO ya muda mrefu yaliyoko kwenye SEKTA ya ELIMU.

MATATIZO hayo ni:

*UMBALI mrefu wanaotembea WANAFUNZI kwenda masomoni

*MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI Madarasani

SULUHISHO:

*UJENZI wa SHULE karibu na MAKAZI ya WANAVIJIJI

*UJENZI wa VYUMBA VIPYA vya MADARASA kwenye Shule zilizopo.

TAKWIMU: SHULE ZA MSINGI

*JIMBO lina KATA 21 zenye jumla ya VIJIJI 68

*SHULE za MSINGI za SERIKALI zipo 111

*SHULE SHIKIZI 12 zinajengwa na kupanuliwa kuwa Shule za Msingi kamili.

*SHULE za MSINGI za Binafsi zipo 3

*VYUMBA VIPYA 395 vya Madarasa vimejengwa ndani ya miaka mitano (2015-2020)

KITONGOJI CHA EGENGE CHAJENGA SHULE SHIKIZI

Kitongoji cha EGENGE ni moja kati ya VITONGOJI vinne (4) vya Kijiji cha BUSAMBA.

Kijiji hicho ni moja ya Vijiji 4 vya Kata ya ETARO. Vijiji vingine ni: Mmahare, Rukuba (Kisiwa) na Etaro.

WANAFUNZI wa Kitongoji cha EGENGE wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 7 kwenda masomoni kwenye Shule ya Msingi Busamba.

UMBALI mrefu na MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani ni sababu kuu zilizofanya KITONGOJI cha EGENGE kiamue kujenga SHULE SHIKIZI yake, na ujenzi ulianza rasmi Mwaka 2016.

MRATIBU wa ELIMU wa Kata ya Etaro, Ndugu Samwel Samike ameeleza kwamba Shule Shikizi hiyo ILIFUNGULIWA Mwaka 2019 na inao WANAFUNZI wa Madarasa matatu, yaani, Darasa la Awali hadi Darasa la Pili.

WINGI wa WANAFUNZI wa Shule Shikizi hiyo ni kama ifuatavyo

*Darasa la AWALI, Wanafunzi 50
*Darasa la KWANZA, 40
*Darasa la PILI, 33.

WANAFUNZI wa Darasa la TATU wa Kitongoji hicho bado wanalazimika kutembea umbali wa zaidi ya kilomita saba (7) kwenda masomoni kwenye S/M Busamba.

UJENZI WA MIUNDOMBINU YA SHULE SHIKIZI

*Vyumba 2 na Ofisi 1 vimejengwa na SERIKALI kupitia Mradi wake wa EQUIP

*Matundu 4 ya choo cha Wanafunzi (EQUIP)

*Matundu 2 ya choo cha Walimu (EQUIP)

*Vyumba 2 na Ofisi 1, SERIKALI kupitia Mradi wa EP4R

*Vyumba 4 na Ofisi 1 vinajengwa na WANAVIJIJI na VIONGOZI wao.

MICHANGO INAYOTOLEWA KWENYE UJENZI HUU

(i) WANAVIJIJI

*Nguvukazi – kusomba mawe, kokoto, maji na mchanga.

*Fedha taslimu – kila KAYA kuchangia Tsh 10,000/=

(ii) SERIKALI – WIZARA ZA ELIMU & TAMISEMI

*Mradi wa EQUIP umechangia Tsh Milioni 60

*Mradi wa EP4R umechangia Tsh Milioni 47.7

(iii) MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo ameanza kutoa MICHANGO yake kwa kuchangia SARUJI MIFUKO 50.

MWENYEKITI wa Kitongoji cha EGENGE, Ndugu Nkuyu Mururi ametoa SHUKRANI nyingi kwa WACHANGIAJI wote ikiwemo SERIKALI yetu.

KIONGOZI huyo anaomba WADAU wa MAENDELEO waendelee kuwachangia VIFAA VYA UJENZI, ambapo MAHITAJI yao kwa sasa ni MABATI 216 na SARUJI MIFUKO 200.

UFAULU WA WATOTO KUTOKA KITONGOJI CHA EGENGE (Darasa la VII 2020)

Kati ya Wanafunzi 53 waliofaulu kutoka S/ M Busamba, Watoto kutoka Kitongoji cha EGENGE wamefaulu saba (7) tu.

Hivyo ni muhimu sana kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza kwa watoto wa Kitongoji cha Egenge – ujenzi wa SHULE SHIKIZI EGENGE ukamilike!

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz