UJENZI WA VIWANGO VIZURI VYA SEKONDARI MPYA YA KATA: MIUNDOMBINU YA MAJI INAJENGWA

MIUNDOMBINU ya KIGERA SEKONDARI ambayo itafunguliwa Mwezi huu (Februari 2021)

Tarehe 8.2.2021.
Jimbo la Musoma Vijijini

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge

KATA ya NYAKATENDE inayoundwa na Vijiji 4 vya Kakisheri, Kamguruki, Kigera na Nyakatende ina SEKONDARI MOJA inayohudumia VIJIJI hivyo na Vijiji vya Kata jirani ya IFULIFU.

Kwa hiyo SEKONDARI moja hiyo inakabiliwa na MATATIZO ya MIRUNDIKANO ya WANAFUNZI madarasani, na wengine wanatembea umbali wa zaidi ya KILOMITA 10 kwenda masomoni.

WANANCHI wa Vijiji 2 (Kigera na Kakisheri) wameamua KUJENGA SEKONDARI yao ambayo itakuwa ni Sekondari ya pili ndani ya Kata hiyo (Nyakatende), na inaitwa KIGERA SECONDARY SCHOOL.

UJENZI WA UBORA WA JUU

AFISA ELIMU na WATAALAMU wa ujenzi wa Halmashauri yetu wanakiri kwamba KIGERA SEKONDARI inajengwa kwa kuzingatia matakwa ya ujenzi yanayotolewa na SERIKALI yetu.

PONGEZI nyingi ziende kwa WANAVIJIJI na WAZALIWA wa Vijiji hivyo, na UONGOZI mzuri na madhubuti wa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kigera, Ndugu Magafu Katura.

MICHANGO YA UJENZI

Michango ya ujenzi wa Sekondari hii inatolewa na:

*WANAVIJIJI – Nguvukazi, yaani kusomba mawe, kokoto, mchanga na maji.

*WANAVIJIJI – Fedha taslimu, Shilingi 2,000 kwa kila MKAZI wa Vijiji hivyo viwili na mwenye umri wa zaidi ya miaka 18.

*WAZALIWA wa Vijiji 2 hivyo. Hawa wanalipa gharama za mafundi na wananunua baadhi ya vifaa vya ujenzi.

*MBUNGE wa JIMBO, Prof Sospeter Muhongo amekwishachangia SARUJI MIFUKO 150 na MABATI 108

*MFUKO wa JIMBO umechangia SARUJI MIFUKO 300 na MABATI 216.

*HALMASHAURI yetu imechangia Shillingi 5,000,000/= (Tshs 5M)

MADAWATI NA SAMANI ZA OFISI

*WAZAZI wa WANAFUNZI 124 watakaoanza masomo KIGERA SEKONDARI wametengeneza Madawati.

*DIWANI wa Kata ya Nyakatende, Mhe Marere Kisha amechangia Samani za Ofisi za Walimu (Viti 8 na meza 4)

MIUNDOMBINU YA MAJI INAJENGWA

*RUWASA inakamilisha ujenzi wa MIUNDOMBINU ya MAJI kwa ajili ya matumizi ya Sekondari hiyo mpya – hii ni sehemu ya MRADI wa RUWASA wa USAMBAZAJI MAJI (kutoka Ziwa Victoria) kwenye Kata ya Nyakatende.

MIUNDOMBINU INAYOKAMILISHWA ILI SEKONDARI IFUNGULIWE

*Vyumba 2 vya Madarasa vimekamilika

*Jengo la Utawala lenye Ofisi 9 limekamilika.

*Boma la CHOO cha Matundu 11. Tundu 1 la choo ni kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalum – limekamilika

*Ujenzi wa CHOO cha WALIMU umeanza.

*Boma la MAABARA 3 linakamilishwa

*Nyumba 1 ya MWALIMU imeanza kujengwa

WANAFUNZI WALIOFAULU KUINGIA KIDATO CHA KWANZA

WANAFUNZI 191 wa Kata ya Nyakatende wamefaulu kujiunga na Kidato cha Kwanza. Hivyo, WANAFUNZI hao 191 watagawanywa kwenye SEKONDARI 2 za Kata hiyo yaani, Nyakatende Sekondari na Kigera Sekondari (itakayofunguliwa Mwezi huu, Februari 2021)

*Vyumba vya Madarasa
*Choo chenye Matundu 11
*Madawati ya Wanafunzi
*Viti na Meza za Walimu
*Miundombinu ya Maji ya RUWASA

ELIMU NI INJINI YA UCHUMI, MAENDELEO NA USITAWI IMARA WA KILA TAIFA

Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini
www.musomavijijini.or.tz