UJENZI NA UBORESHAJI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU WAPANDISHA UFAULU WA SHULE ZA MSINGI

Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

Jumatano, 27.1.2021
Jimbo la Musoma Vijijini

MICHANGO ya WANAVIJIJI, SERIKALI, MBUNGE wa JIMBO na MADIWANI yawezesha Jimbo la Musoma Vijijini na Halmashauri yake kujenga VYUMBA VIPYA 395 vya MADARASA kati ya Mwaka 2015 na 2020.

VYUMBA VIPYA hivyo 395 vimejengwa kwenye SHULE za MSINGI 111 na SHULE SHIKIZI 14.

MUSOMA VIJIJINI YAONGOZA MKOA

Kwa miaka miwili mfululizo (2019 & 2020) Shule za Msingi za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma (Musoma DC) ZIMEFANYA VIZURI na kuongoza Mkoa wa Mara kwenye MITIHANI ya DARASA la NNE (SFNA, standard four national assessment) na Mwaka jana (2020) ufaulu ulikuwa wa kiwango cha 98.04% – PONGEZI NYINGI ziende kwa Wanafunzi, Walimu, Wazazi, DC Dr Anney Naano & Timu yake, na DED Ndugu John Kayombo & Timu yake.

Kwa miaka ya nyuma, Halmashauri yetu ilikuwa inashikilia mkia Mkoani Mara. Haya ni MABADILIKO MAKUBWA yaliyochangiwa na UJENZI na UBORESHAJI wa MIUNDOMBINU ya ELIMU kwenye Shule za MSINGI za Halmashauri hii.

VYUMBA VIPYA VYA MADARASA VYAENDELEA KUJENGWA

Mbali ya ujenzi wa Vyumba vipya 395 ndani ya miaka 5, MBUNGE wa JIMBO na MADIWANI wa Kata zote 21 WAMEAMUA kwamba ifikapo tarehe 1.7.2021, SHULE zote za MSINGI hazitakuwa na MADARASA CHINI ya MITI.

Vilevile, MIRUNDIKANO ya Wanafunzi madarasani itapungua kwa kiasi kikubwa.

WANAVIJIJI wanaomba SERIKALI yao iendelee kuchangia ujenzi wa Vyumba vipya vya Madarasa kwenye Shule zao.

UJENZI WA MAKTABA KWENYE SHULE ZA MSINGI

JIMBO la Musoma Vijijini LINAENDELEA kujenga MAKTABA kwenye Shule zake za Msingi.

MBUNGE wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo anaendelea kugawa VITABU kwenye Shule zote za Msingi na Sekondari. VITABU hivi ni vya Maktaba za Shule na vingi ni vya Masomo ya Sayansi na Lugha ya Kiingereza.

PCI TANZANIA YATOA MICHANGO MIKUBWA

PCI Tanzania inaendelea kuchangia ujenzi wa MAKTABA na utoaji wa VITABU kwenye Maktaba hizo – Ahsante sana PCI Tanzania.

PICHA za hapa zinaonesha:

*Maktaba ya S/M Butata (Jengo lenye rangi ya krimu) – Wanafunzi wakiwa ndani ya Maktaba hiyo.

*Maktaba ya S/M Rukuba (Jengo lenye rangi nyeupe). Hii Maktaba iko Kisiwani Rukuba

*Matokeo ya Darasa la Nne ya Mwaka jana (SFNA 2020) ya Halmashauri 9 za Mkoa wa Mara.

wanafunzi wakiwa ndai ya Maktaba ya S/M Butata

Maktaba ya S/M Butata (Jengo lenye rangi ya krimu) – Wanafunzi wakiwa ndani ya Maktaba hiyo.

Maktaba ya S/M Rukuba (Jengo lenye rangi nyeupe). Hii Maktaba iko Kisiwani Rukuba