KATA YA NYAMRANDIRIRA YAAMUA KUJENGA SEKONDARI YAKE YA KATA

KIKAO kilichofanyika Kasoma Sekondari kilichohudhuriwa na Wananchi wa VIIJIJI 5 vya Kata ya Nyamrandirira, DC wa Wilaya ya Musoma na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini.

Ijumaa, 17.1.2020
Jimbo la Musoma Vijijini
Kata ya Nyamrandirira yenye Vijiji 5 ndiyo Kata kubwa kuliko nyingine zote Jimboni mwetu. Vijiji vyake ni: Chumwi, Kaboni, Kasoma, Mikuyu na Seka.
Kasoma Secondary School ndiyo inatumiwa na Kata hii. Kasoma Sekondari ilianzishwa Mwaka 1995 ikipanuliwa kutoka iliyokuwa “Middle School” ya Serikali iliyoanzishwa Mwaka 1956.
Kasoma Secondary School ina KIDATO V & VI (A-level) cha MASOMO YA SANAA. Jumla ya Wanafunzi wa “A-level” ni 220 ambao wanahitaji Vyumba 7 vya Madarasa. Jumla ya Wanafunzi wa “O-level (Kidato I-IV) ni 929 ambao wanahitaji Vyumba 23 vya Madarasa. Nyumba za Walimu zipo 8 tu kwa Walimu 26 waliopo. UPUNGUFU ni mkubwa (Vinahitajika jumla ya Vyumba 30 vya Madarasa, vipo 24)!
Wanafunzi wa Kata ya Nyamrandirira WALIOCHAGULIWA kujiunga na Masomo ya Kidato cha kwanza Mwaka huu (2020) ni 202. UFAULU huu ni mdogo ukilinganisha na Kata nyingine za Jimboni mwetu.
TAKWIMU hizo hapo juu ZIMESHAWISHI kupatikana  kwa UAMUZI wa kujenga SEKONDARI MPYA ndani ya Kata hiyo badala ya KUENDELEA kuongeza Vyumba VIPYA vya Madarasa hapo Kasoma Sekondari.
Wiki iliyopita, Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Dr Vicent Naano Anney na Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo WALISHIRIKI KIKAO cha WANAVIJIJI wa Kata hiyo kilichotoa UAMUZI wa kujenga SEKONDARI MPYA ndani ya Kata yao.
WANAVIJIJI kutoka VIJIJI 5 vyote vya Kata hiyo WALIKUBALIANA kujenga Sekondari mpya KIJIJINI SEKA.
UJENZI umeanza. DC huyo atasaidia upatikanaji na MAWE na MCHANGA na Mbunge huyo ataanza kutoa MICHANGO yake kwa kutoa SARUJI MIFUKO 100. WANANCHI wa VIJIJI 5 vyote watatoa NGUVUKAZI na MICHANGO mingine ya ujenzi huo.
Vyumba vipya 4 vya Madarasa vinapaswa KUKAMILIKA kabla ya tarehe 30 Machi 2020 ili baadhi WANAFUNZI wa Form I WALIORUNDIKANA Kasoma Sekondari wahamie kwenye Sekondari MPYA inayojengwa Kijijini Seka. Vilevile, kukamilika kwa Vyumba hivyo KUTARUHUSU Kasoma Sekondari kuendelea kutumia MAABARA zake 3 ipasavyo, kwani kwa sasa ndiyo Madarasa ya Form I.
KARIBU TUCHANGIE UJENZI WA SEKONDARI MPYA YA KATA YA NYAMRANDIRIRA.
Mawasiliano ya kutoa MICHANGO:
Mtendaji (WEO)
0683 573 808
M/K Kamati ya Ujenzi
0683 120 444
Katibu Kamati ya Ujenzi
0629 424 717
0767 334 023
SEKONDARI MPYA KUFUNGULIWA JAN 2020 – MAFANIKIO MAZURI
*Busambara Secondary School, Kata ya Busambara (Vijiji 3 – Kwikuba, Maneke na Mwiringo) imekubaliwa kuchukua Wanafunzi wa Form I (2020) wa Kata hiyo.
*Dan Mapigano Memorial Secondary School, Kata ya Bugoji (Vijiji – Bugoji, Kaburabura na Kanderema) imekubaliwa kuchukua Wanafunzi wa Form I (2020) wa Kata hiyo.