MZALIWA WA KIJIJI CHA BUKIMA AANZISHA SHULE YA MSINGI KIJIJINI MWAO – YAZINDULIWA RASMI LEO

UZINDUZI wa AGAPE PRIMARY SCHOOL Kijijini Bukima, Kata ya Bukima. Aliyeshika kipaza sauti ndiye MMILIKI wa Agape Primary School, Ndugu Andrew Kayola.

Wanafunzi, Walimu, Wazazi, Viongozi wa Serikali na Chama (CCM) wamehudhuria SHEREHE za UZINDUZI wa AGAPE Primary School zilizofanyila leo, Jumanne, 7.1.2020 Kijijini Bukima.
KIONGOZI na MMLIKI wa Shule hiyo, Ndugu ANDREW KAYOLE (32yr), mhitimu wa UDOM, Shahada ya Biashara  Bc(HRM) amesema Shule hiyo ilisajiliwa rasmi tarehe 21.6.2017 na tayari WAHITIMU wa kwanza wamemaliza Darasa la 7 (Std 7) Mwaka jana (2019) wakiwa wa KWANZA kwa Wilaya ya Musoma katika kundi lao. Wanafunzi wote walifaulu (A&B). Shule inafundisha kwa lugha ya KIINGEREZA na Mwakani lugha ya KIFARANSA itaanza kufundishwa Shuleni hapo.
MGENI RASMI, Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo amesema kwamba kuwepo kwa Shule Binafsi (Private Schools) Jimboni mwao ni muhimu sana kwa UIMARIKAJI wa UBORA wa ELIMU kupitia USHINDANI KITAALUMA kwa Shule zote za Msingi zilizoko Jimboni humo (Shule 3 za Binafsi na 111 za Serikali).
Mbunge huyo amekuwa AKICHANGIA MAENDELEO ya Shule za Msingi na Sekondari za Serikali na Binafsi bila UBAGUZI wo wote. Aliwakumbusha WAGENI waalikwa kwamba Vyuo Vikuu bora Duniani vimo vya Binafsi (Private Universities) kama vile Harvard (USA),  MIT (USA), Yale (USA) Caltech (USA), na vilevile vimo vya umma (Public Universities) kama vile Oxford (UK) na Cambridge (UK).
Leo, Mbunge huyo amechangia box 10 za VITABU vya Maktaba ya Shule hiyo. Vilevile, amechangia SARUJI MIFUKO 50 kwa ajili ya ujenzi wa Jengo la TEHAMA. Ametoa ahadi ya kuchangia COMPUTER 1 na PRINTER 1 mara Jengo hilo litakapokamilika na kuanza kutumika.
Wakati akizindua AGAPE Primary School na kuweka Jiwe la Msingi la Jengo la TEHAMA la Shule hiyo, Mbunge huyo AMEMWOMBA MWANZILISHI wa Shule hiyo aendelee kuipanua hadi kuanza kutoa MASOMO ya SEKONDARI.
WAZALIWA KUWEKEZA VIJIJINI MWAO
MMILIKI (Ndugu ANDREW KAYOLE) wa Agape Primary School ni KIJANA (32yr) ALIYETHUBUTU na KUFANIKIWA kuwekeza Kijiji mwao. Mbunge wa Jimbo AMEMPONGEZA SANA na kusema JIMBO LINAJIVUNIA kuwa na WAWEKEZAJI wa aina hiyo – TUJIFUNZE KWAKE na TUWEKEZE Vijijini kwetu!