MASHINDANO YA KUPIGA KASIA 2019 (THE ANNUAL BOAT RACE)

VIKOMBE vya WASHINDI na T-SHIRT za Washiriki

Jumapili, 29.12.2019
Jimbo la Musoma Vijijini

KIPAUMBELE Na. 5 (Michezo na Utamaduni) cha Jimbo la Musoma Vijijini kinaendelea kutekelezwa na kesho, Jumatatu, 30.12.2019 kuna MASHINDANO YA KUPIGA KASIA Kijijini Bukima, Kata ya Bukima.

MASHINDANO hayo, kama yalivyo ya KWAYA (Nyimbo), NGOMA za ASILI na MPIRA wa MIGUU ni sehemu ya UTEKELEZAJI wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, ndani ya Jimbo letu (Rejea Kitabu cha Kurasa 110 cha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani hiyo: Januari 2016 – Juni 2019, Jimbo la Musoma Vijijini).

Matayarisho ya MASHINDANO hayo yamekamilika.

MAHALI:
Mwalo (Ufukwe) wa Kijiji cha Bukima

SIKU:
Jumatatu, 30.12.2019

MUDA:
Timu zinazoshindana zitawasili MWALONI (ufukweni) Bukima Saa 2.30 Asubuhi

UKUBWA WA TIMU:
Wapiga kasia 5 kwa kila MTUMBWI (Timu)

USALAMA:
Taratibu za usalama majini (ziwani) zitazingatiwa.

KATA ZILIZOJIANDIKISHA kushiriki kwa ridhaa zao:

(1) Bugwema, (2) Bukima, (3) Bukumi, (4) Bwasi, (5) Etaro, (6) Mugango, (7) Murangi, (8) Musanja, (9) Nyakatende, (10) Rusoli na (11) Suguti

ZAWADI KWA WASHINDI

*Mshindi wa 1
Tsh Milioni 1 & Kikombe

*Mshindi wa 2
Tsh 700,000 & Kikombe

*Mshindi wa 3
Tsh 400,000 & Kikombe

*Kifuta jasho kwa WASHIRIKI ambao hawatashinda: Tsh 50,000 kwa Timu.