MBUNGE MLEZI APANGA HARAMBEE ZA MIRADI YA MAENDELEO

MATUKIO mbalimbali ya KAMPENI za leo (21.11.2019) Jimboni BUTIAMA kwenye Kata za Busegwe na Nyankanga. MGENI RASMI alikuwa Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo ambae ni Mlezi wa Jimbo la Butiama.

Leo, Alhamisi, 21.11.2019, MLEZI wa Jimbo la BUTIAMA, Prof Sospeter Muhongo AMESHIRIKI KAMPENI kwenye Kata 2 za Jimbo la BUTIAMA. Viongozi wa CCM (na Jumuiya zake) wa ngazi za Wilaya, Kata na Vijiji wameshiriki Kampeni hizo wakiongozwa na Ndugu Yohana Mirumbi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Butiama.
KAMPENI hizo zimefanyika kwenye Kata za BUSEGWE (Vijiji 3) na NYANKANGA (Vijiji 2).
MLEZI wa Jimbo hilo ambae ni Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini amewakumbusha WAGOMBEA wa CCM na WANANCHI VIPAUMBELE vilivyo kwenye DIRA yetu ya MAENDELEO na umuhimu wa KUTEKELEZA ILANI ya Uchaguzi ya CCM (2015-2020) kwa umakini mkubwa.
WAGOMBEA wa CCM wakiongozwa na Wenyeviti wa Vijiji 5 vya Kata hizo mbili, WAMEAHIDI kuanza na kuendeleza utekelezaji wa MIRADI ya MAENDELEO kwa kasi kubwa baada ya Uchaguzi wa tarehe 24.11.2019.
WANANCHI na WAGOMBEA wa CCM wamepanga kupiga HARAMBEE, tarehe 28.11.2019 ya kuendeleza ujenzi wa SEKONDARI ya Kata ya Busegwe.
Tarehe 30.11.2019, WANANCHI na WAGOMBEA wa CCM wamepanga kupiga HARAMBEE ya kupanua Shule SHIKIZI ya Nyabange iwe SHULE ya MSINGI yenye Shule ya Awali hadi Darasa la VII.