WANANCHI WA KIJIJI CHA KABURABURA NAO WAAMUA KUJENGA ZAHANATI YAO

Wananchi wa Kijiji cha Kaburabura, Kata ya Bugoji wakisomba MCHANGA, kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati yao.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
Wananchi wa Kijiji cha Kaburabura kilichoko Kata ya Bugoji WAMEAMUA na KUANZA UJENZI WA ZAHANATI YA KIJIJI chao.
HUDUMA za AFYA kwa WAKAZI wa Kijiji cha Kaburabura ZINAFUATWA kwenye VIJIJI JIRANI, yaani Kijiji cha Bugoji, umbali wa kilomita 4 au Kijiji cha Kangetutya, umbali wa kilomita 5, kwenye Wilaya nyingine, Wilaya ya Bunda.
Jumatano, tarehe 4.9.2019 WANAVIJIJI hao wameanza ujenzi wa Zahanati ya Kijiji chao baada ya KUFANYA UAMUZI wa pamoja.
Aidha hatua za ujenzi wa Zahanati hiyo umeanza chini ya Usimamizi wa Mwenyekiti wa Kijiji cha Kaburabura Ndugu Chriphord Masatu, na Kaimu VEO Ndugu Majura Magambo.
Akifafanua juu ya ujenzi huo, Ndugu Chriphord Masatu ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji hicho, amesema kuwa, kazi za Ujenzi wa Zahanati hiyo zitafanyika JUMANNE na ALHAMIS ya kila wiki, huku wakitaraji kukamilisha ujenzi huo ndani ya takribani MIEZI 4 na ifikapo Januari 2020, ujenzi uwe umekamilika.
Ndugu Masatu ameendelea kufafanua kuwa mbali na NGUVUKAZI za WANANCHI za kusomba Mawe, Kokoto, Mchanga na Maji ya ujenzi,  WAMEKUBALIANA kwamba KILA KAYA ichangie Tsh. 50,000/= (Elfu hamsini) ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika mapema.
Kazi hizo za  AWALI za usombaji wa mchanga, zimeongozwa na Katibu wa CCM wa Tawi la Kaburabura Ndugu Juma Magoti.
Diwani wa Kata ya Bugoji, Mhe Ibrahimund Malima wamewaomba Wananchi wa Kijiji hicho kushirikiana vema ili kuhakikisha ujenzi unakamilika kama ulivyopangwa.
Diwani huyo pia ametoa wito kwa WAZALIWA wa Kijiji cha Kaburabura walioko nje ya Kijiji hicho, KUSHIRIKIANA na  Ndugu, Jamaa na Marafiki zao walioko Kijijini hapo, KUKAMILISHA MRADI huu muhimu sana kwa Huduma Bora za Afya zao.
Diwani huyo ametoa taarifa kwamba Group la WhatsApp liitwalo, “KABURABURA NI KWETU,” ndilo Group LINALOWAUNGANISHA Wazaliwa wa Kijiji cha Kaburabura na Rafiki zao kwenye UTEKELEZAJI wa Mradi huu na mingineyo.
Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo AMETOA PONGEZI nyingi kwa WANA- KABURABURA kwa UAMUZI wao huo mzuri na ATAENDA KUPIGA HARAMBEE ya ujenzi huo na yeye mwenyewe atachangia SARUJI MIFUKO 100.
ILANI YA CCM ya UCHAGUZI ya 2015-2020 INATEKELEZWA kwa KASI kubwa kwenye Jimbo la Musoma Vijijini:
*Zahanati Mpya 14 zinajengwa Jimboni kwa NGUVUKAZI za Wananchi na Michango ya SERIKALI na WADAU wengine wa Maendeleo
*Kituo cha Afya 1 (Kata ya Nyambono) kinajengwa.
*Hospitali 1 ya Wilaya, Kitongoji cha Kwikonero, Kijiji cha Suguti inajengwa.
HUDUMA ZA AFYA ZITOLEWAZO JIMBONI
*Zahati 24 za Serikali
*Zahanati 4 za Binafsi
*Vituo vya Afya 2 (Murangi na Mugango)
ILANI YA CCM: Kila Kijiji kiwe na Zahanati Moja – Jimbo la Musoma Vijijini lenye Vijiji 68 linatekeleza KWA VITENDO.