VIJANA WANUFAIKA NA KILIMO CHA BUSTANI KWA KUTUMIA FEDHA ZA MFUKO WA JIMBO

baadhi ya Wanakikundi cha NYAKABHUNGO wakiwa kazini kwenye BUSTANI yao ya MBOGAMBOGA iliyoko Kijijini Kanderema, Kata ya Bugoji.

Na: Hamisa Gamba
Msaidizi wa Mbunge
KILIMO CHA UMWAGILIAJI, kikiwemo cha BUSTANI za mbogamboga na mazao mengine kinazidi kushamiri ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini.
VIJANA na Wananchi wengine kwa ujumla wameendelea kunufaika na aina hii ya KILIMO tofauti na kile kilichozoeleka cha kutegemea MVUA.
VIJANA wa Kikundi cha NYAKABHUNGO GROUP kilichoko kwenye Kijiji cha Kanderema, Kata ya Bugoji ni moja ya Vikundi vilivyopewa MASHINE/PAMPU za Kilimo cha Umwagiliaji na MBEGU kutoka MFUKO wa JIMBO ambao Mwenyekiti wake ni Mbunge wa Jimbo.
KIKUNDI hiki kinanufaika na MSAADA huo kutoka Serikalini (Mfuko wa Jimbo) na VIKUNDI vingine vinavyofanya vizuri ni:
(ii) Angaza, Kata ya Bukumi
(iii) Mwanga Farmers, Kata ya Nyambono
(iv) No Sweat No Sweet, Kata ya Bwasi
(v) Mkulima Jembe, Kata ya Bukima
(vi) Keuma, Kata ya Busambara
(vii) Jitume, Kata ya Suguti
Mwenyekiti wa Kikundi cha NYAKABHUNGO,  Ndugu Mtaka Mwenura,
ameeleza kuwa Kikundi chao kinajishughulisha na Kilimo cha NYANYA, VITUNGUU, MBOGAMBOGA, MAHINDI na VIAZI VITAMU na kwamba wanataraji kuingia sokoni hivi karibuni.
Mwenyekiti huyo,  kwa niaba ya VIJANA wa Kikundi hicho wameishukuru sana SERIKALI kupitia Mbunge wao wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo na HALMASHAURI yao, kwa kutoa Vifaa hivyo vya Kilimo cha Umwagiliaji.
Diwani wa Kata hiyo,  Mhe Ibrahimund Malima ametoa shukrani za kipekee kwa Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo, Mkuu wa Wilaya, Dr Vicent Naano Anney na Mkurugenzi wa Halmashauri yao, Ndugu John Kayombo kwa UTEKELEZAJI mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM (2015 – 2020).
Diwani huyo anamshukuru sana Mbunge wao wa Jimbo kwa KUGAWA BURE Mbegu za ALIZETI kwa misimu 3 mfululizo. Kwa sasa ALIZETI ni zao jipya la BIASHARA linalolimwa Jimboni humo.
Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, anaendelea kutoa wito kwa VIJANA, KINAMAMA na WATU WENYE ULEMAVU waendelee kuunda VIKUNDI vinavyotambulika kwa ajili ya kupata MIKOPO, pale fursa inapotokea.