UJENZI, UKAMILISHAJI NA UBORESHAJI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI KWENYE SEKONDARI ZA KATA

Ufyatuaji wa Matofali 1,200 kwa ajili ya UKAMILISHAJI wa ujenzi wa BOMA lenye Maabara za Masomo ya Sayansi ya Sekondari ya Murangi.

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Jimbo la Musoma Vijijini lina jumla ya Sekondari 18 za Kata/Serikali na 2 za Binafsi (Katoliki & SDA). Sekondari Mpya 8 zinajengwa Jimboni mwetu.
Kazi mojawapo muhimu INAYOFANYWA kwa wakati huu ni UJENZI, UKAMILISHAJI na UBORESHAJI wa MAABARA za MASOMO ya Sayansi (Physics, Chemistry na Biology)  kwenye Sekondari zetu za Kata.
Sekondari zote 20 (za Serikali na Binafsi) zina VITABU vya kutosha vya Masomo ya SAYANSI vinavyogawiwa na Mbunge wa Jimbo, Prof Sospeter Muhongo. Mbunge huyu anahimiza ujenzi wa Maktaba kwenye Shule zote za Sekondari na Msingi.
MAABARA ZA SEKONDARI YA MURANGI
VIJANA Wazaliwa wa Kata ya Murangi yenye Vijiji 2 (Lyasembe na Murangi), wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Mhe Kujerwa Simon Kujerwa, WAMEAMUA kuchangia SARUJI MIFUKO 70 kwa ajili ya kuanza kazi za UKAMILISHAJI  wa BOMA lenye Maabara 3 za Masomo ya SAYANSI kwenye Sekondari ya Kata yao, yaani Murangi Secondary School.
Ujenzi huu ulisimamia Mwaka 2016 na Diwani huyo ambae ameingia madarakani hivi karibuni, AMEFUFUA ujenzi huo na nia yao sasa ni kukamilisha Boma hilo lenye Maabara zote tatu.
Mwalimu Mkuu wa Secondari ya Murangi, Mwl Ernest Mazoya amemshukuru sana Mhe Diwani huyo KUFUFUA ujenzi wa Maabara zao. Sekondari hiyo ilifunguliwa Mwaka 2006.
Awali akitoa taarifa ya ujenzi huo, Diwani huyo amesema kwa SASA Wananchi wa Kata ya Murangi WAMEKUBALI kuchangia NGUVUKAZI zao kwa kusomba mchanga, mawe, kokoto na maji ya ujenzi. Vilevile, Wananchi hao WAMEKUBALI kuchangia gharama za MAFUNDI.
Mhe Kujerwa Simon Kujerwa anawashukuru sana Vijana wenzake waliojitokeza kuchangia ujenzi wa Maabara hizo. Kwa hatua hizi za awali MICHANGO imetolewa na VIJANA waishio ndani ya Kata hiyo ambao ni:
(1) Magesa Saile
(2) Kalii Saile
(3) Magoti Biswaro
(4) Robert Kainja
(5) Soti Mashenene
(6) Thomas Kujerwa
(7) Mea Nyang’ombe
(8) Nyandeka Gesi
(9) Sabina Nyamayugu, na
(10) Diwani mwenyewe
Ofisi ya Mbunge wa Jimbo INAENDELEA kuwashawishi WADAU mbalimbali na hasa WAZALIWA wa Jimbo la Musoma Vijijini KUENDELEA KUCHANGIA Maendeleo ya Kata zetu 21 na Vijiji vyetu 68. Kila Kijiji kina MRADI wa Maendeleo unaotekelezwa kwa wakati huu – KARIBU UCHANGIE.