KIJIJI CHA NYASAUNGU WATUMIA WIKI 1 KUKAMILISHA MSINGI WA SEKONDARI WANAYOIJENGA

kazi za ujenzi wa Msingi (foundation) wa Sekondari ya Kijiji cha Nyasaungu kilichoko kwenye Kata ya Ifulifu

Na: Fedson Masawa
Msaidizi wa Mbunge
Taarifa ya awali ya UJENZI wa SEKONDARI ya KIJIJI cha NYASAUNGU, Kata ya Ifulifu, ilitolewa tarehe 14.06.2019.
Baada ya WIKI MOJA, tayari MSINGI (foundation) wa Jengo la kwanza umekamilika. Jengo hilo ni la Vyumba Vitatu (3) vya Madarasa.
Kwa Mujibu wa Kamati ya Ujenzi wa  Sekondari hiyo, ifikapo Jumamosi, tarehe 22.06.2019, JAMVI litamwagwa.
MICHANGO YA UJENZI WA SEKONDARI YA KIJIJI
Wakazi wa Kijiji cha Nyasaungu WANACHANGA kati ya Tsh 200,000 na 40,000 kutoka kila KAYA.
MICHANGO imegawanywa katika MAKUNDI 4 kama ifuatavyo:
(i) Kundi la WAFUGAJI wenye NG’OMBE kati ya 10 na 29, kila KAYA inachangia Tsh 50,000/=
(ii) Kundi la WAFUGAJI wenye NG’OMBE kati ya 30 na 50 kila KAYA inachangia Tsh 100,000/=
(iii) Kundi la WAFUGAJI wenye NG’OMBE kati ya 51 na 200, kila KAYA inachangia Tsh 200,000/=
(iv) Kundi lenye KAYA ZISIZO na NG’OMBE  au zenye NG’OMBE chini ya 10, zinachangia Tsh 40,000/=
Mbali ya MICHANGO wanayoendelea kutoa, NGUVUKAZI za Wanakijiji hao zinatumika kusomba mawe, kokoto, mchanga, maji na kufyatua tofali.
NYASAUNGU NGUVU MOJA, KARIBUNI TUCHANGIE MAENDELEO YA KIJIJI CHA NYASAUNGU