ELIMU YA KILIMO SHULENI – SHULE YA SEKONDARI NYANJA YAANZA KUTOA ELIMU YA KILIMO CHA ALIZETI KWA WANAFUNZI WAKE

Wanafunzi wa Sekondari ya Nyanja WAKIPALILIA zao la ALIZETI kwenye SHAMBA la SHULE

Jumamosi, 15.06.2019
Na: Verediana Mgoma
Msaidizi wa Mbunge
Shule ya Sekondari Nyanja, ilioyoko Kata ya Bwasi, imeanza kutoa ELIMU ya KILIMO cha ALIZETI ili  kuandaa  VIJANA KUJIAJIRI WENYEWE kwenye Sekta ya Kilimo mara wamalizapo Masomo ya Kidato cha IV na wengine wavutiwe KUSOMEA fani ya KILIMO waendeleapo na MASOMO ya juu.
Mwalimu Charles  Ndebelle ambae ni Mkuu wa Sekondari  ya Nyanja ameeleza kwa namna ambavyo Shule hiyo imechukua uamuzi wa kujishughulisha na KILIMO ili kukuza PATO na UCHUMI wa SHULE kupitia KILIMO huku wakitumia FURSA hiyo KUELIMISHA na KUANDAA WANAFUNZI wao kuingia kwenye AJIRA na UTAALAMU wa KILIMO kwa siku zijazo.
Mwalimu Mkuu huyo amesema kwamba maeneo yote ya Shule yalio wazi yatapandwa MAZAO mbalimbali na wanatarajia kuanza KILIMO CHA UMWAGILIAJI hivi karibuni kwani Sekondari ya Nyanja iko umbali wa mita 200 kutoka Ziwa Viktoria.
Afisa Kilimo wa Kata hiyo ya Bwasi, Ndugu Gustavu Msahi ameongeza na kusema kwamba sehemu ya MAFUNZO ya KILIMO shuleni hapo ni yale ya kuwajengea uwezo na uzoefu WANAFUNZI  kutambua umuhimu wa MAZAO ya muda mfupi  ya CHAKULA (k.m. mbogamboga) na ya BIASHARA (k.m. ALIZETI).
Afisa Kilimo huyo ameeleza kwamba MASHAMBA ya hapo Shuleni yanatumika kama SHAMBA DARASA kwa JAMII inayoishi karibu na Sekondari hiyo.
Aidha Diwani wa Kata  ya Bwasi Mhe Masatu  Nyaonge  amewashauri WALIMU wa Sekondari ya Nyanja kuendelea kuboresha SOMO la KILIMO na kuanza kulitoa kwenye Shule za Msingi zilizo jirani nao.
VIONGOZI hao, yaani Diwani, Afisa Kilimo na Mwalimu Mkuu wa Sekondari ya Nyanja kwa pamoja WAMEMSHUKURU SANA Mbunge wa Jimbo lao, Prof Sospeter Muhongo kwa KUSIMAMIA VIZURI uanzishwaji wa Kilimo cha ALIZETI Jimboni humo. Mbunge huyo AMEGAWA BURE Mbegu za ALIZETI kwa Misimu ya Kilimo 3  mfululizo ikiwa ni Jumla ya taribani TANI 10 za Mbegu za ALIZETI alizonunua yeye  mwenyewe na TANI 10 nyingine alizopewa na Serikali. Sekondari ya Nyanja iligawawiwa bure Mbegu za ALIZETI za Mbunge wao.
Vilevile, Mbunge Prof Muhongo ALISHAGAWA BURE Mbegu za MTAMA, MIHOGO na alishirikiana na Halmashauri kusambaza bure Mbegu za UFUTA.
Sekta ya KILIMO, kikiwemo Kilimo cha Umwagiliaji, inaimarishwa ndani ya Jimbo la Musoma Vijijini ili kutoa AJIRA kwa Vijana na Wanavijiji wengine, kupambana na upungufu wa CHAKULA, na kupanua wigo wa Mazao ya Biashara (pamba, alizeti, mihogo, n.k.) Jimboni humo.